Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
'msione soo kujikosha'

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema wakati umefika kwa
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutooneana
aibu katika kukisafisha chama hicho ili kifanye kazi
iliyokusudiwa na wanachama wake.

Kauli hiyo aliitoa katika mkutano wa hadhara baada ya
ufunguzi wa tawi la CCM la Chuo Kikuu cha Tumaini
lililopo Kihesa nje kidogo ya mji wa Iringa.

Pamoja na kuagiza wana-CCM kutooneana haya, alisema
kumuita mtu fisadi kama kweli ni fisadi si mbaya,
kwani ni njia ya kuondoa uozo uliopo kupisha sera za
chama kufanya kazi zake.

"Kama ni kweli umeiba fedha za umma, wewe ni fisadi
tu hakuna haja ya kubadilisha jina..." alisema Waziri
Mkuu huyo huku akiimbiwa wimbo wa “Sema Pinda
usiogope, sisi vijana hatuogopi vibaraka.”

"Kila mmoja ajitazame mwenyewe... nimewekwa na
wananchi, iweje nianze kuwaibia" alisema Waziri Mkuu
huku akisisitiza kwamba CCM si mafisadi, bali wapo
watu wenye mapungufu na hao ni lazima washughulikiwe.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.