Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Nazir awasilisha vielelezo

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir
Karamagi, aliyejiuzulu amewasilisha vielelezo kwa
Spika kuthibitisha kauli aliyoitoa bungeni kwamba
kuongezwa kwa mkataba wa TICTS ni makubaliano ya
Baraza la Mawaziri.

Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam na
kuthibitishwa na Kaimu Katibu wa Bunge, Dk Thomas
Kashililah zinasema kuwa Karamagi amewasilisha
vielelezo hivyo ndani ya siku saba kama alivyoagizwa
na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samwel Sitta.

Dk Kashililah alisema kuwasilishwa kwa vielelezo
hivyo kunampa fursa Spika wa Bunge kuvipitia kwa
makini na kuandaa hukumu ambayo ataisoma katika Bunge
lijalo la Bajeti.

Spika wa Bunge Samwel Sitta alimtaka Karamagi
kuwasilisha vielelezo hivyo ndani ya siku saba baada
ya kushindwa kufanya hivyo katika kikao cha Bunge
lililomalizika wiki iliyopita.

Spika alitoa agizo hilo baada ya Karamagi kuwasilisha
barua kwake, akisema waraka wa kikao cha Baraza la
Mawaziri aliotakiwa kuuwasilisha Bungeni kuhusiana na
mkataba wa TICTS, ni wa siri hivyo hawezi
kuuwasilisha na kwamba, anachoweza kukifanya ni
kunukuu maelezo ya kikao cha baraza hilo na kisha
kuomba apewe muda aitafute na kuiwasilisha bungeni
katika mkutano ujao.

Ombi la Karamagi halikukubaliwa na badala yake
alimtaka awasilishe uthibitisho huo ndani ya siku
saba kuanzia siku kilipomalizika kikao hicho hadi
vinginevyo atatumia kanuni za Bunge kumchukulia
hatua.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.