Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Nami ndani ya ufunguzi wa Taifa Cup!

Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa ufunguzi wa michuano Kombe la Taifa, inayoanza kutimua vumbi siku za karibuni hapa hapa nyumbani katika Uwanja wa Taifa.



Michuano hiyo huendeshwa kwa mtindo wa mtoano na inashirikisha mikoa 23 ya soka Tanzania Bara.

Katika mchezo wa ufunguzi utakaofanyika kati ya Iringa na Manyara, naye Waziri Mkuu Pinda anatarajiwa kufungua michuano hiyo.

Pia siku ya ufunguzi huo litakuwepo kundi maarufu la vichekesho la hapa nchini la Ze Comedy, likiambatana na bendi ya Msondo kwa ajili ya kutoa burudani kwa watazamaji watakaofika uwanjani kushuhudia pambano hilo.

Pia wakazi wa Dar es Salaam na mikoa mingine ya jirani wameombwa kujitokeza kwa wingi, ili kushuhudia michuano hiyo itakayokuwa ni ya msisimko na mvuto juu yao.

Pia zile timu za Iringa, Manyara, Tanga, Kagera, Kigoma na Ruvuma zilizopangwa kucheza mwanzoni mwa ratiba hiyo ya michuano, zitaanza kuingia jijini leo tayari kwa mashamulizi hayo.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.