Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Nyuki wamvurugia JK

Mapokezi ya Rais Jakaya Kikwete wilayani Iramba yalikumbwa na mkasa wa nyuki waliotanda katika eneo la shule ya Sekondari Kinyangiri na kusababisha kushindikana kuwekwa kwa jiwe na uzinduzi wa shule hiyo.

Hali hiyo ilitokea baada ya msafara wa rais kufika eneo la shule hiyo maalumu kwa ajili ya kuzindua shule na kuendelea na mkutano wa hadhara nje kidogo ya eneo la shule hiyo.

Baada ya msafara huo kufika nyuki walitanda eneo zima na kufanya rais ashindwe kushuka katika gari lake kwa dakika tano kabla ya kuondoka na kwenda pembeni na kuingilia mlango wa nyuma wa jengo la utawala la shule hiyo ambalo lilitumika kupokea taarifa ya wilaya hiyo.

Hata hivyo, baada ya kupokea taarifa ya wilaya hiyo, nyuki hao walijikusanya pembeni kidogo mwa miti ambayo ilikuwa imezunguka sehemu lilipojengwa jiwe la uzinduzi, hali iliyosababisha uzinduzi huo kutofanyika.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.