Spika sasa kulimwa maswali.
Spika wa Bunge sasa atakuwa akizungumza na waandishi wa habari kila mwezi ambapo ataulizwa maswali mbalimbali yanayohusiana na utendaji wa ofisi yake.
Ofisi ya Bunge imeanzisha utaratibu huo mpya kama hatua ya kukuza uhusiano kati ya vyombo vya habari na taasisi hiyo pekee ya kutunga sheria hapa nchini.
Utaratibu huo mpya ulitangazwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila, alipokuwa akifungua warsha ya waandishi wa habari za Bunge.
Akizungumza katika warsha hiyo iliyolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuzijua zaidi taratibu na kanuni mbalimbali za Bunge,Kashilila alisema licha ya utaratibu huo mpya wa kukuza uhusiano, lakini pia hiyo itakuwa ni fursa ya pekee kwa wanahabari kujua masuala
mbalimbali yahusuyo Bunge.
Kashilila alisema utaratibu huo ambao utakuwa ukifanyika wakati wa kifungua kinywa (Coffee meeting), unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu, na kwamba utaruhusu pia mawaziri kujumuika na Spika ili kwa pamoja waweze kuzungumzia mambo muhimu yanayohusu utendaji
kazi wa serikali na majukumu ya Bunge.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala