vipanya vyashukiwa kwa msongamano.
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imekataa kusajili na kutoa leseni kwa magari ya kusafirisha abiri (daladala) 3,800 aina ya vipanya, katika hatua yake ya kuhakikisha kuwa vyote vinaondolewa katikati ya jiji.
Afisa Mfawidhi wa Sumatra Kanda ya Mashariki,Walukani Luhamba alisema hivi sasa hawasajili vipanya kwa kuwa havitakiwi katikati ya Jiji.
Alisema hatua ya kutosajili vipanya hivyo ni moja ya mkakati wa kupunguza msongamano barabarani kwa kuwa vinasababisha kero kwa abiria na watumiaji wengine wa barabara.
Alisema hivi sasa Sumatra ina mkakati wa kutafuta na kusajili mabasi makubwa yanayoweza kubeba abiria wengi na kwamba hadi sasa tayari yapo mabasi 10 yanayotoa huduma hiyo sehemu mbalimbali jijini.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala