Walimu wa msingi kula shavu.
Rais Jakaya Kikwete, amesema walimu waliochukuliwa kutoka shule za msingi kwa ajili ya kufundisha sekondari, wataendelea kuwa walimu wa sekondari.
Alitoa maelezo hayo wakati akihutubia wakazi wa Kiomboi, wilayani Iramba kwa mujibu wa Rais Kikwete, walimu hao ni wenye stashahada.
"Nasikia mnawaita walimu wa kuazima, hawa si wa kuazima tena, hawatarudi kufundisha shule za msingi, wajue kuwa ndiyo wamefika,” alisema.
Kuhusu taratibu nyingine za uhamisho, Rais alisema mamlaka zinazohusika serikalini zitashughulikia suala hilo.
“Taratibu nyingine za mchakato huo wa kuwabakisha kuwa walimu wa kudumu wa sekondari tutakamilisha sisi wenyewe,” alisema.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala