Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Iringa ni noma Taifa cup.

Michuano ya Kombe la Taifa ambayo mwaka huu inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ilifunguliwa rasmi jana Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam huku Iringa ikiipa dispilini Manyara mabao 4-1.

Katika mchezo huo Iringa ilionenyesha kufunika wapinzani wao, ambapo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 2-1.

Iringa ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa dakika ya nne na Yusuph Peter, ambapo dakika ya 16 aliongeza la pili kabla ya Manyara kupata bao dakika ya 16 mfungaji akiwa Sunday Muchee kwa penalti baada ya Bunda Oden kumchezea vibaya Hamis Mponzanyema.

Bao la tatu la Iringa lilifungwa dakika ya 60 na Jeremiah Juma akiunganisha krosi ya Rashid Juma, huku la nne likifungwa tena na Juma dakika ya 90. Yusuph Peter alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Waziri Mkuu ndie aliyekuwa mgeni rasmi ambapo aliwataka wanamichezo kuhakikisha wanafanya vizuri na kwamba itakuwa ni aibu kuwepo kwa Uwanja mpya wa kisasa wa Taifa kama Watanzania hawatapata nafasi ya kushiriki michuano mikubwa badala yake uwanja huo utumiwe na
wageni.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alikifagilia kikundi cha Ze Comedy na kusema kuwa sanaa ikitumiwa vizuri inaweza kuleta ajira ya kubwa kwa wahusika.

Alisema ni vyema viongozi wengine wakachukulia mambo yanayosemwa na wasanii hao kama changamoto ya kuboresha udhaifu wanaouelezea na wasikasirike wakielezwa ukweli.

Aliwachekesha wapenzi wa soka waliokuwepo uwanjani hapo, baada ya kueleza kwamba huwa anatizama anavyoona Waziri Mkuu anavyoigizwa na kwamba jana alifanikiwa kukutana na waigizaji hao 'live'.




 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.