Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Chenge asanzuka kwao kujikosha.

Baada ya kukumbwa na tuhuma nzito za ufisadi, Andrew Chenge, sasa ameamua kwenda jimboni kwake Bariadi Magharibi, kujikosha kwa wapigakura wake.

Mtindo kama huo ulitumiwa pia na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ambaye baada ya kujiuzulu katika mkutano wa 10 wa Bunge la Februari alikwenda jimboni kwake Monduli ambapo alipokewa na watu na magari mengi, kitendo ambacho kilitafsiriwa kuwa alikuwa anajisafisha kutokana na kashfa ya Richmond.

Ziara hiyo ya Chenge kwenda jimboni ni ya kwanza tangu aanze kuchunguzwa na makachero wa Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza ya Serious Fraud Office (SFO).

Uamuzi huo wa Chenge pia kufanya ziara jimboni kwake umekuja ikiwa ni wiki moja baada ya kuzushiwa kifo.

Habari zilizopatikana kutoka jijini hapa zilisema Chenge alitarajiwa kuwasili Bariadi jana usiku akitokea Mwanza.
Taarifa hizo ziliongeza kwamba, Chenge ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu baada ya kukutwa na Sh1.2 bilioni katika akaunti yake katika kisiwani Jersey, zinazohusishwa na biashara ya kifisadi ya rada, pia atawaeleza wananchi wake sababu za kujiuzulu kwake.

Habari zaidi zilieleza kwamba, Chenge atakwenda katika jimbo hilo ambako baadhi ya watu wanaojiita wafuasi wake wamemwandalia mapokezi makubwa ya kumsafisha na tuhuma za ufisadi zinazomkabili.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.