Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
JK ashtukia usanii wa mkwanja wake.

Rais Jakaya Kikwete amesema baadhi ya maofisa wa benki zilizoidhinishwa na Serikali kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo nchini kupitia mfuko maalumu, maarufu kama ‘mabilioni ya JK’, wamejichotea mabilioni hayo kwa kujikopesha huku wakiwatelekeza walengwa.

Amekerwa na mfumo wa benki hizo kuficha taarifa za wakopaji pindi zinapotakiwa na watendaji waandamizi wa Serikali, wakiwamo wakuu wa wilaya na kufafanua kuwa, maadili hayo ya kuficha taarifa za wateja, hasa wakopaji yanatumika vibaya na maofisa hao ili wasibainike kuwa
wamejikopesha.

Katika kudhihirisha kuwa amekerwa na tabia hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa Serikali ndiye mdhamini mkuu wa wakopaji hao, alisema “Tutabanana” ili mambo yaende sawa.

Rais Kikwete alionyesha kutoridhishwa na hali hiyo wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ya siku tano mkoani Singida, katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi.

“Tatizo la benki ni kukataa kutoa taarifa za wakopaji kwa viongozi wa Serikali. Wanainyima taarifa Serikali. Mie natoa fedha yangu uwape watu.

Nikikuuliza mwenendo wao unanieleza ni siri. Wakuu wa wilaya wanataka kujua nani amekopeshwa na ukweli ni kwamba tuliowakopesha tumewadhamini sisi (Serikali) kwa nini hatupati taarifa? “Tutazungumza na wakuu wa benki kuona namna ya kupata ufumbuzi wa suala hili...Tutakwenda kubanana ili hatimaye tuweze kupata taarifa.

Kuna wilaya moja siitaji, meneja wa benki na wenzake wakakopeshana Sh bilioni 1.2 wakajigeuza wajasiriamali,” alisema.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.