Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Judo TZ yapigwa tafu.

Chama cha Judo TZ (JATA), kinatarajiwa kupokea msaada wa vifaa kutoka Shirikisho la Mchezo wa Judo barani Ulaya (EJU), kwa ajili ya kuendeleza mchezo huo, ikiwa ni maandalizi ya mashindano ya kimataifa mwakani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa JATA, Kashinde Bundala aliyoitoa kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera wakati wa uzinduzi wa klabu ya michezo ya judo na karate wilayani Korogwe, iitwayo Korogwe Budokan.

Alisema msaada huo tayari umeishawasili nchini,ambapo JATA inajiandaa na mashindano ya dunia yatakayofanyika Septemba 2009, jijini Amsterdam nchini Uholanzi.

Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa CCM mjini Korogwe, uliongozwa nahodha wa timu ya taifa ya judo Tanzania, Sensei Zaidi Hamisi, ambaye alifuatana na wachezaji wenzake kutoka Dar es Salaam.

Kashinde alimweleza Waziri Bendera kuwa, kabla ya kwenda Uholanzi mwakani, timu ya taifa itakayokuwa na wachezaji watano na kiongozi mmoja kutoka JATA, Julai mwaka huu watakwenda Ureno kujipima nguvu na miamba ya nchi hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Waziri Habari na michezo Joel Bendera aliwataka wachezaji hao kutambua kwamba, mchezo huo ni sawa na michezo mingine ambayo inapendwa duniani, hivyo wajitahidi kupata vijana wenye nidhamu na bidii ya kuuendeleza mchezo huo.





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.