Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
MP asutwa.

Jumuiya ya Ulaya (EU) imemsuta Mbunge wa Tarime, Chacha
Wangwe (Chadema), aliyetaka kuihusisha Jumuiya hiyo na vitendo vya rushwa ambavyo vimeibuka nchini hivi karibuni.

Hali hiyo ilitokea kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa maendeleo nchini unaofadhiliwa na EU kwa zaidi ya mbovu zipatazo bilioni 952 kwa miaka sita. Uzinduzi huo ulifanyika Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo, Wangwe, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema, aliwashangaza watu waliohudhuria baada ya kuishutumu Jumuiya hiyo kuwa inashirikiana na serikali kufanya ufisadi.

Alitoa shutuma hizo alipouliza swali kwa Balozi Clarke baada ya balozi huyo kusema anaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali kuhusu ufisadi.

“Nashangaa kuona unasema serikali inajitahidi kupambana na
ufisadi, sijui habari hizi umezipata wapi… hii haitashangaza kama tukisema na nyinyi mnahusika na ufisadi pamoja na serikali,” alisema

Akijibu tuhuma hizo, Mwakilishi wa Tume ya Ulaya (EC), Balozi Tim Clarke alisema anashangazwa na tuhuma kwamba wao wanajihusisha na ufisadi, wakati wao siku zote wamekuwa wakipigania kuimarika kwa vyombo kama Bunge ili vidhibiti viongozi wasiokuwa waadilifu.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.