Simba,Yanga kupumua!
Kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea leo katika viwanja mbalimbali nchini, huku miamba ya soka nchini Simba na Yanga ikiwa benchi hadi Septemba 13 mwaka huu.
Mchezo mwingine utafanyika ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ukiikutanisha Toto African dhidi ya Moro United, ambapo Toto katika mchezo wa kwanza iliifunga JKT Ruvu bao 1-0 huku Villa Squad ikipachika mabao yake mabao 3-2 ndani ya lango la Azam.
Kivumbi kingine kitakuwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma, wakati Polisi ya mhini humo itakapokuwa mwenyeji wa Azam, mchezo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute.
Septemba 6 wakati Toto African itakapoikaribisha Kagera Sugar Polisi Dodoma itakuwa mwenyeji wa Moro United, huku JKT Ruvu ikivaana na Azam Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Miamba ya soka nchini Simba na Yanga, haitakuwa na mechi katika ligi hiyo hadi Septemba 13, wakati Simba itakapokuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya kuikabili Prisons na Yanga itakuwa Jamhuri Morogoro kuchuana na Mtibwa Sugar.
Simba na Yanga zimeahirishiwa michezo yao kutokana na kuwa na wachezaji wengi kwenye kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kilichoingia kambini jana kujiandaa na mchezo dhidi ya Mauritius Jumamosi ijayo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala