Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Stars kuelekea Mauritius leo!

Kikosi cha Timu ya Taifa Taifa Stars kinatarajia kutimua leo nchini kuelekea Mauritius, kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kufuzu kushiriki kwenye fainali za Mataifa ya Afrika CAN) na zile za Kombe la Dunia.



Mchezo huo kwa Taifa Stars ni wa kukamilisha ratiba baada ya timu hiyo kuwa na pointi mbili.

Mchezo huu utapigwa siku ya Jumamosi huko Mauritius, Taifa Stars inauchukulia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mchezo muhimu wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Fredrick Mwakalebela alisema kwamba Taifa Stars ilirejea nyumbani jana ikitokea Bulyanhulu, Shinyanga ambako iliweka kambi ya mazoezi kwa siku tatu.

Mwakalebela alisema katika safari hiyo Stars itaondoka na wachezaji 18, wakiwemo na viongozi sita na mashabiki 17 watakaokwenda kuishangia timu hiyo.

Wachezaji wako katika morali ya juu na wanangojea mchezo wa Jumamosi, lengo lao hasa ni kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

Kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo alisema atakitumia kikosi kilichoshuka katika dimba la uwanja mpya wa kisasa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Ghana ‘Black Stars’ katika mchezo huo kwani Taifa Stars na Ghana walitoka sare ya bao 1-1.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.