Kareti kukunjana mwezi huu
Hatimaye yale Mashindano ya Kareti kwa upande wa vijana wenye umri chini ya miaka 16, yanatarajia kuwasha moto Septemba 27 ndani ya viwanja vya Don Bosco hapa jijini.
Daniel Mbega ndiye Mwenyekiti wa Klabu ya Scorpion Shotokan, alisema kwamba mashindano hayo yatajumuisha wachezaji kutoka Zanzibar ikiwemo na Kenya.
Mashindano hayo yatashirikisha klabu sita kutoka Tanzania Bara, na nyingine zitatoka Zanzibra na Kenye kwani lengo ni kupima uwezo wa wachezaji.
Mwenyekiti huyo alisema mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kila mwaka, ikiwa kama mwendelezo wa kukuza vipaji kwa wale wenye uelewa na mchezo huo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala