Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Mashangingi yabaniwa serikalini.

Serikali inafanya marekebisho makubwa ya namna ya udhibiti wa uendeshaji wa magari ya kifahari kwa mawaziri na viongozi wengine kuondokana na matumizi mabaya ya mali za umma.

Hayo yamo katika ripoti ya Mpango wa Serikali kuhusu Orodha ya Magari yake na Kudhibiti Matumizi ambayo imependekezwa pamoja na mambo mengine magari ya kifahari ya mawaziri maarufu kama mashangingi yanunuliwe kila baada ya miaka saba badala ya miwili ya sasa.

Utaratibu wa sasa ni kwamba, gari la waziri huweza kununuliwa kila baada ya miaka miwili tangu linunuliwe na kuanza kutumika, kisha hutumiwa na watendaji wa ngazi ya chini, au kuuzwa au waziri.

Takwimu za sasa, gari moja aina Toyota VX au Toyota GX, hadi kuliingiza nchini ni kati ya Sh 80 hadi 120 milioni ambayo ni kwa ajili ya serikali, huku gharama za operesheni ikiwa ni pamoja na matengenezo ya kila wiki na mafuta ni kati ya Sh moja hadi 1.5 milioni, kutegemea safari.

Ripoti hiyo ya kitaalamu ambayo inalenga kuishauri serikali namna ya kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma katika ununuzi na uendeshaji magari ikiwemo hayo ya kifahari, katika mapendekezo yake inaonyesha pia haja ya kupunguzwa kwa orodha hiyo ya magari kwa kiwango cha nusu.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.