'Michuma vimeo si ruksa'.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha ameagiza Polisi nchini kuwachukulia hatua kali madereva wanaosababisha ajali ili kudhibiti wimbi la ajali zilizokithiri nchini.
Katika hotuba yake wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi yaliyofanyika Chuo cha Polisi Barabara ya Kilwa Dar es Salaam, Masha pia ameliagiza jeshi hilo kukamata na kuyaondoa magari yote mabovu barabarani kwa kuwa nayo yanachangia kiasi kikubwa matukio ya ajali nchini.
“Kumekuwa kukitokea ajali nyingi hapa nchini siyo tu kwa sababu ya uendeshaji mbaya, bali pia kuwapo kwa magari mabovu barabarani. “Kimsingi hatuwezi kuwadanganya wananchi kwani wao pia wanayaona.
Kwa kupitia fursa hii napenda Jeshi la Polisi lenye heshima kubwa sasa, litende yale wananchi wanayoyategemea,” alisema Masha.
“Kwa mantiki hiyo, ningependa madereva wanaovunja sheria za barabara na kusababisha vifo visivyo na lazima, wachukuliwe hatua kali na magari mabovu yote yasiyostahili kuwa barabarani yasionekane.
” Waziri pia aliwaagiza wahitimu waliomaliza mafunzo na askari wengine wote kufanya kazi kwa bidii na maarifa waliyopata kuhakikisha kuwa maisha ya watu hayapotei kwa sababu ya ajali barabarani.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala