Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Netiboli kufufuliwa!

Kumekuwa na upendeleo sana katika mchezo wa mpira wa miguu 'soka', kwani watanzania wengi wamekuwa wakipaisha sana mpira wa soka na kuweza kuipa kisogo michezo mingine.



Mbali na hilo pia mchezo wa netiboli umekuwa ukipewa kisogo sana, kwani hapo awali ulikuwa uko juu sana na kupendwa na wengi.

Wanawake wamekuwa wakitengwa kwa kupewa nafasi ya mwisho katika suala zima la ufadhili.

Kwani baadhi ya makampuni yanajumuika kwa pamoja sasa kuufufua mchezo huo wa netiboli, ili kuweza kuwaridhisha wanawake na kuwapa kipaumbele zaidi katika suala zima la mchezo huo.

Pia viongozi wa Chama Cha Netiboli Tanzania (CHAHETA) wanatakiwa kulitembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano, ili waweze kutoa ushawishi wa kutosha kwa wanachama wa Chama cha Wabunge wanawake ili mchezo huo unyanyuliwe.





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.