Wafanyakazi Muhimbili watulizwa!
Mgomo wa wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili umechukua sura mpya baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wilson Mukama kuwaeleza wafanyakazi hao kuwa madai yao yatalipwa mwisho wa mwezi huu.
Pamoja na majibu hayo, wafanyakazi hao ambao juzi walitishia kufanya mgomo mkubwa Jumatatu ijayo kama hawatalipwa malimbikizo ya mishahara kuanzia Januari hadi Juni na mishahara mipya kuanzia Julai mwaka huu, wametishia kugoma kuanzia kesho.
Awali Mukama aliyefika katika hospitali hiyo jana mchana kuzungumza na wafanyakazi baada ya uongozi wa hospitali hiyo chini ya Mkurugenzi, Profesa Leonard Lema, kutaka kauli ya serikali kuhusu madai hayo, alipata wakati mgumu kuhutubia kutokana na kila wakati ukumbi wa mkutano kugubikwa na kelele.
Alisema malipo ya watumishi wa sekta ya afya hasa taasisi yamebadilika mwaka huu na sasa mishahara tachukuliwa moja kwa moja na taasisi husika kutoka Hazina badala ya kupitia wizarani, jambo lililosababisha ichelewe.
Mukama aliwahakikishia kuwa malipo ya mishahara yao pamoja na malimbikizo yamekamilika na utaratibu wa kupeleka orodha ya malipo kutoka taasisi hiyo inatakiwa kufanyika Septemba 13, baada ya ile iliyopaswa kufanyika Agosti kuchelewa kutokana na waraka wa mabadiliko hayo
kutoka baada ya Agosti 13.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala