Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Wanasiasa watakiwa kuacha usanii.

Wanasiasa wametakiwa kuacha kujitafutia sifa na badala yake wawe wakweli kwa wananchi ili mipango ya kuinua hali zao za maisha ifanikiwe.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Lephy Gembe wakati akizungumza na wataalamu wa kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kumpa taarifa za mipango ya serikali ya kumwezesha mkulima masikini kupata pembejeo kwa kutumia hati punguzo kwa kasi zaidi.

Gembe alisema baadhi ya mipango ya serikali inatibuliwa kiutendaji na wanasiasa ambao wanataka kujipatia sifa bila kuwaelimisha wananchi kuwa wanatakiwa kujipanga huku wakisaidiwa na serikali.

"Wapo wanaotaka kusema kwamba wananchi waiachie serikali kufanya kila kitu, hii si sawasawa… wananchi wanatakiwa waelekezwe kujitegemea tangu mapema,” alisema Mkuu huyo wa wilaya na uongeza kuwa haitafaa kitu kujipatia sifa za kijinga na kukwamisha wananchi kujitegemea.

Timu ya wataalamu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ipo Nyanda za Juu Kusini kutoa hamasa ya matumizi sahihi ya mbolea ya minjingu, matumizi ya hati punguzo, sensa ya wakulima na namna mpya ya uwakala wa mbolea ya ruzuku na ufundishaji mawakala.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.