Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Mkwanja wa bajeti wamiminika

Uingereza imekuwa nchi ya kwanza kati ya wafadhili 14 wa mfuko wa Bajeti Kuu ya Serikali (GBS), kuchangia mfuko huo kwa kutoa Sh bilioni 216 na wafadhili wengine wanatarajiwa kutimiza ahadi zao ifikapo Desemba mwaka huu.

Kwa Serikali ya Uingereza kutoa fedha hizo, kunazima mjadala uliokuwapo kwamba wafadhili hao wamekataa kutoa fedha hizo kwa sababu mbalimbali yakiwamo madai kwamba serikali haijachukua hatua ipasavyo katika masuala mbalimbali yakiwamo ya ufisadi.

Fedha hizo, Sh bilioni 216 ni asilimia 25 ya Sh bilioni 810 zinazotegemewa kutolewa na wafadhili kutoka nchi 14 hadi kufikia Desembamwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema fedha hizo zimeingizwa katika akaunti ya Benki Kuu iliyopo London Uingereza kwa paundi milioni 103.5 ambazo ni sawa na Sh bilioni 216.

Alisema nchi hiyo ya Uingereza ni moja kati ya wahisani 14 wanaochangia katika Mfuko wa Bajeti Kuu ya Serikali, wengine wakiwa ni Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Canada, Denmark, Finland, Ujerumani, Japan, Ireland, Tume ya Ulaya, Uholanzi, NorwaySweden, Uswisi na Benki
ya Dunia (WB).

“Fedha zilizotolewa na Uingereza ambao ndio wachangiaji wakubwa katika Mfuko huo wa Bajeti Kuu ya Serikali ni asilimia 25 ya fedha zote ambazo zinatarajiwa kutolewa katika mfuko huo ambapo wahisani wengine watatoa fedha walizoahidi katika kipindi cha miezi sita kwa mujibu
wa makubaliano ili serikali iendelee na programu zake,” alisema Mkulo.

Alisema Bajeti ya Serikali inategemea wahisani kwa asilimia 12 tu na iwapo itajumuishwa na mikopo mbalimbali katika shughuli za maendeleo kama ujenzi wa barabara na maji, ndio inafikiainafikia asilimia 34, hivyo si kweli kuwa bajeti inategemea wahisani kwa asilimia 34.

Hivyo kwa namna hiyo, aliwataka Watanzania kutambua kuwa si kweli kuwa kuna nchi wahisani zimekataa kutoa fedha katika Mfuko wa Bajeti Kuu kwani wana kipindi cha miezi sita wakiendelea kutoa michango yao na si kweli kuwa bajeti itashindikana kukamilika.

Alisisitiza kuwa serikali inajiendesha kwa uhuru na utaratibu waliojiwekea chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, hivyo hakuna nchi inayoweza kuweka masharti ya kufanya jambo fulani ndipo watoe misaada







 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.