Zidane, Carlos, Scholari,Gullit kuja tz!
Wale nyota wa soka duniani Zinedine Zidane, Robert Carlos, Ruud Gullit akiwemo na kocha wa timu inayoongoza Ligi nchini England, Chelsea, Philippe Scholari wanatarajiwa kutua nchini kwa madhumuni ya kukuza soka hapa nyumbani.
Nyota hao watakuja baada ya kuweka saini mkataba na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mpaka sasa wamekwishawasilisha ombi lao TFF juu ya mpango huo.
Kwani ujio wa nyota hao kutawapa fursa vijana kujifunza kutoka kwao, na kuitangaza nchi kimataifa.
Hii itakuwa ni nafasi nzuri kwa wale vijana ambao wanataka kujiendeleza kisoka, kwa kufanya mahojiano na nyota hao na kujua siri ya mafanikio yao katika soka.
Kwani TFF imeonyesha nia ya kutaka kufanya kazi nao endapo watakubaliana na shirikisho hilo, itabidi wawahakikishie usalama wa nyota hao kabla ya kuwaleta hapa nyumbani.
Katika mpango wao kampuni hiyo yenye makao makuu Uholanzi, inatarajia kufungua shule ya soka itakayochukua watoto 400 wenye vipaji ambavyo vitakuwa chini ya ukurugenzi wa kocha wa kimataifa.
Nyota hao wameamua kuelekeza nguvu zao hapa nyumbani baada ya kugundua kuwa kuna vipaji vingi vya soka, ambavyo vinahitaji kuboresha kabla ya kwenda kucheza mpira wa kulipwa.
Kituo hicho cha soka kitakapo funguliwa kitafundisha vijana katika kiwango kinachotakiwa, wataleta mawakala wa wachezaji kutoka timu kubwa barani Ulaya kuja kuwachagua na kuwapeleka kwenye majaribio.
Mbali na hiyo, pia wataandaa vipindi vya televisheni kwenye vituo mbali mbali vya kimataifa, ambavyo wana mikataba navyo, vitakavyozungumzia soka la Tanzania na kuonyesha baadhi ya wachezaji kwa kuweza kuinua nchi kwa ramani ya soka.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala