Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Nakuja na 'Mwanzo Mwisho'

Si mwigine ali ni yule Kocha Mkuu wa timu ya soka Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Marcio Maximo, alisema matunda ya timu yake sasa yameanza kuonekana kuchipua na kuzionya timu nyingine kukaa mbali.



Alizitaka timu nyingine kukaa mbali na timu yake, kwani amesema kwanzia sasa anakuja na progarmu mpya iitwayo Mwanzo Mwisho, itakayoifanya timu hiyo kupaa zaidi.

Kocha huyo alisema atahakikisha timu yake inaendeleza kasi iliyoanzisha ya ushindi, baada ya juzi kuilaza Msumbiji bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani dhidi ya Sudani.

Alisema pamoja na mambo mengine katika programu hiyo ya Mwanzo Mwisho, anatarajia kuliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuitafutia timu yake michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa ili kujiweka fiti.

Katibu Mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela alisema timu hiyo itaendelea na kambi yake, huku ikijiandaa na mchezo wa Sudani utakaofanyika Novemba 29 mwaka huu hapa hapa nyumbani.

Na ule wa marudiano utakaofanyika nchini Sudani Desemba 14 mwaka huu.

Mbali na hilo pia Kipa timu ya Yanga Juma Kaseja leo anatarajia kufunga ndoa na Nasra Nassoro jijini Dar es Salaam.

Hiyo ni ndoa ya kwanza ya kipa huyo tofauti na taarifa za baadhi ya vyombo vya habari kuwa alipata kumuoa aliyekuwa mtalaka wa kiungo mahiri nchini, anayechezea pia Yanga, Athumani Idd.

Kwani wachezaji wa Taifa Stars watashuhudia ndoa hiyo, ambapo wamepewa ruhusa maalum na kutakiwa baada ya ndoa kujikita kambini.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.