Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
IGP:Hakuna upendeleo kwa vigogo EPA

Vigogo waliosalia kwenye sakata zima la tuhuma za wizi wa fedha kwenye akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), nao pia kwenda kuonja joto ya jiwe mahakamani.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali (IGP) Said Mwema, alisema hakuna cha salia mtume hapa na hakuna wa kupona EPA, kwani sheria itafuata mkondo wake juu ya watuhumiwa hao.

Kauli hiyo Kamanda huyo ni ya tatu kutolewa na wajumbe wa Timu ya Rais ya EPA, kwani tayari Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliazer Feleshi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) Edward Hosea, wameonya kwamba hakuna mtu aliyehusika na tuhuma hizo atakayepona.

Akijibu swali Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kuhusu kwa nini hadi sasa vigogo wa EPA hawajakamtwa, na ni lini watafikishwa mahakamani? IGP Mwema, alisema wale wote waliojikombea fedha za akaunti hiyo wako njiani kufikishwa mahakamani.

Alisema Vigogo ni wakina nani? kwani kesiinaendelea na wanaofikishwa mahakamani ni wale ambao taratibu muhimu zinazohitajika zimekamilika na wengine watafikishwa mahakamani, taratibu zikikamilika.

Mwema alisema hakuna mtu atakayeonewa na kwamba, wahusika wote watafikishwa katika vyombo vya sheria kwa mujibu wa katiba, zitafuata mkondo wake.

IGP akizungumzia mchakato huo mzima na kitisho kutoka kwa baadhi ya watuhumiwa wa EPA kwa mahakimu wa Kisutu, alikiri kuwepo kwa hali hiyo kwani tayari malalamiko yamefika katika ofisi yake.

Kwani malalamiko ya mahakimu hao yanatokana na kile walichokiita kwamba, ni kutishiwa usalama wao kutokana na kazi zao katika uendeshaji wa kesi za EPA.

"Sisi jeshi la polisi tuko pamoja nao na kuhakikisha hawapati madhara kutokana na vitisho hivyo wawapo kazini na sehemu nyingine,"alisisitiza Mwema.

Kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi hairuhusu mtu, watu, ama kikundi kuvuruga amani kwa makusudi kwa maslahi yao binafsi.

Alisema suala la amani na utulivu nchini ni muhimu sana kwani jeshi lake limeamua kufanya uchunguzi, kufuatia malalamiko ya wanafunzi ya kupigwa na kufanyiwa fujo katika migomo inayoendelea.

"Tunasisitiza kwamba, demokrasia ipo na iendelee kuwepo, lakini iende sambamba na kuwepo kwa amani na utulivu," alihoji.

Kwa mgandamizo alisema jeshi hilo liko karibu na viongozi wa wanafunzi, na kutaka kupewa taarifa kama kuna wanaochochea migomo hiyo ya wanafunzi wa vyuo nchini.

Suala la EPA na migomo ya wanafunzi ni mambo ambayo hadi sasa yanaivaibrati nchi, kufuatia kuwepo na mvutano kutoka kwa wadau mbalimbali, serikali na vyombo vya dola.

Wakati watu wakitaka vigogo zaidi wa EPA wakamatwe na kufikishwa mahakamani, hadi sasa bado kuna ukimya huku kwa upande wa migomo ya vyuo vikuu serikali ikiamua kuvifunga na vyombo vya dola kukamata baadhi ya wanafunzi kwa tuhuma za uchochezi.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.