Walimu:'No pay No game'
Baadhi ya walimu ambao majina yao hayakutoka katika orodha ya serikali ya majina yaliyohakikiwa, waliweza kuandamana na kujikusanya katika ofisi za Manispaa ya Temeke na Kinondoni wakitaka waelezwe hatima ya madai yao.
Mwalimu mwingine aliyejitolea kuzungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema majina yaliyobandikwa hapo Kinondoni ni zaidi ya 300.
Kwani walimu hao wanatarajia kukuta fedha hizo zimeingia kwenye akaunti zao leo, lakini cha kushangaza majina yao hayapo na mpaka sasa hawajajua hatma yao.
Alisema hawajui sababu za majina yao kutotoka kwa kuwa takribani wote walitakiwa kuandika barua kwa Ofisa Elimu wa manispaa zao ambayo inaorodhesha madai yao jambo ambalo wamefanya.
Kutokana na hali hiyo waliamua kwenda kumuona Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, ili wapate ufafanuzi lakini waliishia nje baada ya kuambia kuwa viongozi hao hawapo wako nje ya ofisi.
Kwa mujibu wa mmoja wa maofisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambaye alidai si msemaji, alisema kutotoka kwa majina hayo si tatizo kwa kuwa yanatoka kwa awamu kwani majina ni mengi na mengine bado yanaendelea kuhakikiwa.
Baadhi ya walimu walisema hawakupenda majina yao kutajwa, walisema wamefurahishwa na kitendo hicho kwani sasa wanaamini haki na madai yao ya muda mrefu yatakuwa yamelipwa.
Kwani Serikali imesambaza kiasi cha Sh bilioni 12 katika wilaya mbalimbali nchini, kwa ajili ya kulipa madeni ya walimu yaliyohakikiwa.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala