Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Warioba: Ulafi ndiyo unaowapanza

Kumekuwa na mmomonyoko mingi ikiibuka chinichini kwamba, viongozi wengi wamekuwa wakithamini zaidi mali kuliko maslahi ya wananchi.

Hayo yalisemwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Jaji Joseph Warioba, alisema alitamani sana Azimio la Arusha lirudi kwa kile alichokielezea na kukiona.

Alisema imefika kipindi sasa wananchi kutotegemea sheria kuwa itajenga msingi wa maadili kwa viongozi, bali matendo yao ndio yatajenga maadili hao ambayo yanafanya mpaka kuwemo na Azimio la Arusha la pili ili kulinda maadili hayo.

Warioba huyo alisema iwapo Azimio hilo la pili litarudi na hali ya sasa ya maadili ya viongozi itabadilika, na matatizo mengi hasa ya ufisadi yatakwisha.

“Suala la maadili ya viongozi historia yake inaanzia zamani ambako, viongozi walikuwa wakijali zaidi maslahi ya wananchi kwa kufuata misingi ya Azimio la Arusha.

"Pengine kwa sasa umefika wakati wa Arusha nyingine ambako, viongozi kama sisi tutakuwa na ujasiri wa Arusha ya 1967,” alisema Warioba.

Alisema bila vitendo vinavyoambatana na maadili sheria ni bure, kwani uongozi huambatana na kujitolea na kujali zaidi.

Kwani viongozi wa kipindi hicho cha zamani walikuwa wakifuata maadili yao pamoja na miiko, iliyopo ndani ya azimio hilo ambayo ni kama ukitaka kuwa kiongozi ni lazima uwe mkulima au mfanyakazi usiwe na hisa katika kampuni yoyote, usiwe mkurugenzi wa bodi au kampuni binafsi, usiwe na mishahara miwili na usiwe na nyumba ya kupangisha.

Jaji Warioba alisema Azimio la Arusha lilikuwa linazingatia kuwa fedha si msingi wa maendeleo bali ni matokeo, hali ambayo kwa sasa ni kinyume.

Kwani sasa fedha imekuwa ndio msingi wa uongozi, kwani ndio unaoonekana kuwa njia ya kujitajirisha kama ilivyo kwa sasa.

Kutokana na hali hiyo kumekuwa na matabaka ambapo mkulima na mfanyakazi sasa hawana tena nafasi ya kuwa viongozi, bali wenye mali au wenye uhusiano wa karibu na wenye mali.

Alisema kwa sasa hali ni ngumu, kwani matabaka yanaonekana wazi viongozi wengi wanaonekana kujali maslahi yao zaidi. “Sasa hivi kima cha chini ni 100,000 wakati mshahara wa juu kabisa ni mamilioni, zamani viongozi walikuwa tayari kutoa uamuzi mgumu kupunguza mishahara yao, tofauti na sasa”.

Jaji Warioba kuwa ni kiongozi makini ambaye amekuwa mstari wa mbele kusimamia maadili tangu kipindi cha awamu ya kwanza, na yupo wazi kukosoa kwa vile anavyoamini yeye hali ambayo inapaswa kuigwa na viongozi nchini.





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.