Eti waliosaini mikataba tata wafungwe!
Ile kamati ya Bunge ya Miundombinu imeishauri serikali ya Jk kuacha kucheka na watendaji walioliingiza Taifa katika mikataba tata...na iwachukulie hatua kali ikiwemo kuwaburuza selo.
Ukiachilia hilo kamati hilo linaloongongwa na Mwenyekiti wake, Mh.Mohammed Missanga,pia imeitaka Serikali kuvunja mkataba wake na Kampuni ya RITES ya India (TRL) kwa kushindwa kutimiza wajibu wake wa kuboresha shirika hilo badala yake kutafuna fedha za wananchi.
“Tatizo la msongamano wa makontena katika Bandari ya Dsm kamati inaishauri Serikali kufanya maamuzi na kutekeleza maazimio ya Bunge yaliyotolewa katika Mkutano wa 11 kuhusu marekebisho ya baadhi ya vipendele vya Mkataba wa TICTS vyenye mapungufu.
“Kusitisha nyongeza ya miaka 15 iliyoongezwa bila kufuata Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004, kuondoa ukiritimba wa TICTS na kufungua wigo wa huduma hiyo bandarini na kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria wote walioiingiza Serikali kusaini mikataba yenye upungufu kama huu wa TICTS,”alisema Bw. Missanga.
Wakati Kamati hiyo ikiitaka Serikali kusitisha mkataba wake na TICTS, wadau wa Bandari hiyo wakiwemo wamiliki wa Bandari Kavu (ICD) wameutupia lawama uongozi wa TICTS kwa kushindwa kuwajibika na kudharau hata agizo la Rais Jakaya Kikwete la Januari mwaka huu kuhusu kumaliza mrundikano wa makontena bandarini hapo.
Wadau kadhaa walioongelea mrundikano wa makontena bandarini na 'kuwafukuza' wafanyabiashara wengi kwenda nchi jirani ni ukiritimba wa TICTS kukataa kuhamisha makontena katika Bandari Kavu.
“Ili TICTS wapate pesa waliamua kuweka ukiritimba wa kuchelewesha utoaji
makontena na kuyahamisha katika bandari kavu ili waweze kuvuna hizo dola kwa siku, hiki ndicho kiini hasa cha mrundikano wa makontena bandarini, sasa baada ya Mh. Rais kuona hali ya mrundikano huo, alituita Ikulu Januari mwaka huu na tukakubalina kwamba kazi ya TICTS ni kupokea na kutoa makontena na si kuhifadhi (storage).

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala