Deni lawakwamisha mapacha walioungana!
Deni lawakwamisha mapacha walioungana kutoka Hospitali Kuu ya Nairobi inawashikilia mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana baada ya wazazi wao kushindwa kulipia huduma ya uzazi.
Habari zimeeleza kuwa, hadi sasa imefikia miezi 16 tangu mapacha hao wazaliwe na wazazi wao ambao ni wakimbizi kutoka Somalia waishio nchini Kenya.
Kwa mujibu wa mama wa mapacha hao wa kike, Anab Hussein, ameliambia shirika la habari la BBC kuwa familia yake inadaiwa zaidi ya dola za Marekani 30,000 na hospitali hiyo ya Kenyatta huku deni hilo likiongezeka kila siku.
Amesema kuwa, kadiri siku zinavyozidi kuongezeka ndivyo mzigo unavyozidi kupanda na wala hafahamu deni hilo watalilipa vipi.
Amesema kuwa, hospitali moja nchini Marekani tayari imekubali kujaribu kuwatenganisha, lakini hawawezi kuruhusiwa kusafiri hadi watakapokuwa wamelipa deni lao.
Kutokana na hali hiyo, imeelezwa kuwa, raia wa Somalia waishio nchini Kenya wameanza kupokea michango ili kuwasaidia mapacha hao waweze kuondoka hospitalini.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala