Ukurasa
huu: Maskani
/ Gari la Waziri,linapobeba BANGI toka Tarime!
Gari la Waziri,linapobeba BANGI toka Tarime!
Wauzaji na wasambazaji wa bangi nchini Kenya,wamebuni mbinu mbadala ktk kufanikisha usafirishaji wa bangi kutoka Bongo pande za Tarime ambapo inaaminika ndiko kunakozalishwa bangi nyingi kuliko sehemu yoyote uliyowahi kuisikia kwa kipande hiki cha mashariki ya afrika.
Sasa unaambiwa kipande cha muda kidogo wajinga hao walitinga pande za tarime wakiwa na ndinga (gari) la naibu waziri flani aliyejulikana kwa jina la Oburu Odinga..huku ndinga hiyo ikiwa na plate namba za serikali.
Lengo haswa la wafanyabiashara hawa kutumia gari hilo ni kuepuka kuzuiliwa bila mpango na askari wa usalama kila wanakokatiza.
Cha kushangaza ktk sakata hili wajinga hawa walifanikiwa kukatiza kipande chote cha bongo toka Tarime bila kunaswa kwa kutumia njia zao a panya..lakini wakaja naswa na polisi wa hukohuko kwao. Fwatilia kisanga kizima ktk video hii hapo juu iliyonaswa na wanoko flani wa nchini humo.
Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!! Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!