Kili Marathon 2010 hiyoo
Kwani wameweza kuthibitisha kitendo cha kushiriki kwenye mashindano ya riadha ya Kilimanjaro Marathon, kwa mwaka huu yamepangwa kuwika hapo Februari 28 ndani ya Uwanja wa MUCCoBS hapa mjini.
Si wengine bali ni wale Wanariadha maarufu wa hapa nchini watashiriki kwenye mashindano hayo, na yatakuwa ni mashindano ya nane huku yakiendelea kuchipua vipaji vipya huku yakiwataja wanariadha wazoefu waliothibitisha mpaka sasa.
Washiriki hao ni pamoja na Patrick Nyangero, Jumanne Tluway, Samwel Kwaang akiwemo na Banuelia Brighton.
Naye Katibu Msaidizi wa Riadha Tanzania (RT) Julius Musomi alisema Nyangero alifanikiwa kumaliza kwa kushika nafasi ya pili kwenye mshindano hayo hapo mwaka jana kwenye mbio za Marathoni kwa kutumia saa 2:15:35.
Mbali na Nyangero kushika nafasi hiyo ya pili, pia Tluway aliyekuwa mshindi hapo mwaka juzi, kwa mwaka jana aliwezamaliza huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Andrea Silvini saa 02:16:22.
Kwaang aliibuka kidedea ya mbio za nusu Marathoni hapo mwaka jana, huku Brighton ndiye anashikilia rekodi ya taifa kwa wanawake tangu mwaka juzi kwa kushinda mbio za marathoni.
Musomi alimtaja pia Mary Naali ambaye ni kati ya wanariadha bora wa kike hapa nchini kuwa amethibitisha kushiriki mbio za mwaka huu.
Wanariadha wengine wanaotarajiwa kushiriki ni pamoja na Fabiola William, Mashaka Masumbuko, Mekiadi Bayo, Restituta Joseph, Sarah Maja, Faustine Musa, Samson Ramadhani, Damian Chopa, Ezekiel Ngimba na Sarah Kavina.
Musomi amewaombWanariadha wengine kutoka Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida na sehemu nyingine za hapa nchini wameombwa kujitokeza kwa madhumuni ya kushiriki katika mashindano hayo ambayo huwa na zawadi mbalimbali zikiwemo zile za fesha.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala