Kimiti awavunja mbavu wabunge kisa FATAKI!
Wabunge wanaoudhuri kikao cha bunge la jamhuri ya Tz asubuhi ya leo mjini Dodoma walijikuta hawana mbavu kwa vicheko baada ya mzee wetu mbunge wa siku nyingi Mh.Paul Kimiti (Sumbawanga Mjini) kusimama na kuomba jina 'Fataki' lisitumike kama linavyotumika hivi sasa kwani linamfedhehesha kutokana na ukweli kuwa babu yake anatumia jina hilo.
Jina fataki limekuwa maarufu mjini likiwa linatumiwa na jamaa mmoja kwenye tangazo angalizi la vita dhidi wakware wanaolaghai wanafunzi na watoto wadogo wa kike kimapenzi.
Sawa mzee kimiti...sasa kwa kuwa babu yako anaitwa fataki unataka tubadilishe mpaka matangazo yetu...lakini tushasikia kuna mtu anaitwa dume..je na wale watengeneza wa kondom aina ya dume si na wao watatakiwa kubadilisha jina hiloooo..kaaaazi

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala