Tafuta DHWTangazaTuandikie
Ni mdogo kiumri lakini .........

NI mmoja kati ya wabunge wadogo kiumri bungeni lakini mwenye mawazo nachangamoto kushinda hata watu wazima bungeni ambao ye anawaita baba ,mama na babu kama si bibi zake.


Amina Chifupa Mpakanjia


Akiwa na wa miaka 25 tarai alishavikwa ubunge wa vijana wa kuchaguliwa kwa kura wa wajumbe wa ccm

Akielezea historia yake kwa ufupi Amina Chifupa Mpakanjia anasema alianza kusoma shule ya msingi ya Ushindi,kisha akajiunga na shule ya sekondari ya Kisutu kala ya kuhitimu kidato cha sita katika shule ya Makongo na kuhitimisha elimu yake katika Chuo cha uandishi wa Habari cha Royal College.

Akiwa Shule alianza kazi ya utangazaji wa Redio hadi alipokuja kuutwaa Ubunge ndipo alipozidiwa na majukumu ya ubunge na kuamua kupumzika utangazaji.

Analo lililomsukuma yeye kuingia katika siasa na si kwamba kuna mtu alimshawishi yeye aingie kwenye siasa.....mie mwenyewe ndiye niliyeamua kuingia kwenye siasa ila baada ya kuona baba yake yaani mzee Chifupa ambaye amekuwa mwanasiasa wa muda mrefu...alieleza Amina


Mbali na kufuata nyayo za babaabgu pia ile dhana ya kuonekana wanawake hawawezi ndo kilichoniingiza mimi na kunipa mie nguvu ya kugombea uongozi...ni katika kuonyesha hata sie wanawaweke twazeza

japo si mashindano ila ni nia ya kuonyesha kuwa uwezo upo...na pia wanawake kama getrude mongela,daftari...condoleza rice nao walinichochea saana mie kuingia katika uongozi.

Amina ambaye ni mama wa mtoto mmoja...anasema pia anasema, aliona ana deni la kuitumikia Tanzania..... especial vijana wenzangu...nikaona mie kama kijana ninauwezo wa kuwawakilisha vijana wenzangu sio hadi nifikie miaka 40,sasa nani atawasemea vijana matataizo ya vijana yanatatuliwa na vijana wenyewe sababu ndio wanajua matatizo yao .

uzoefu wa uongozi

nilikuwa monito, kiranja, vikundi mbalimbali ya masuala ya shule ambayo yaliniandaa vya kutosha

Nikiwa nina miaka 18 nilitamani kuingia katika siasa ila, baba alinikataaza kwa kniambia mie bado mdogo ila nilijiunga kwa kukata tiketi ya uanachama ambako kupitia huko nilipata ...kuwa kamanda wa vijana


Amina alielezea ni kwanini alichagua CCM na si vyama pinzania....nae aliwakuwa na haya ya kusema ....ni chama tawala. kimenilea, kimenisomesha sababu baba angu alikuwa anaitumikia ccm na ameshawahi kushika nafasi za juu alishawahi kuwa naibu mkurugenzi wa uchaguzi 2002...

Hivyo sikuwa nasababu ya kwenda upinzani sababu nilikiamini,,,,halafu nahisi upinzani haujakomaa, kwani ni vichanga, vina mogogoro, vina pandikiza udini...pia nikamkumbuka mwalim nyerere ambaye alikuwa anasisitiza umoja bila kujali udini,ukabila

ccm, inajali ina nafasi za vijana, walemavu, wazee, watoto,,,niliona hakuna ubaguzi nikilinganisha na vyama vingine ndipo nilipoamua kuchagua ccm

Nilitaka kujua ni kitu gani alihisi kilimpa ushindi akijilinganisha na wagombea wenzie?

Sababu kubwa waliona ninafaa. kwani nilifanya kampeni nchi mzima tz na visiwani kwa kukutana na wajumbe na kuwaeleza nia yangu , na jitihada zangu ndio zilipekea mie kuchaguliwa

na nyengine nilizipata siku ya kupiga kura baada ya kujieleza na kuwashawishi kwa sera zangu.....mengine wanajua wao nia zao zakunichagua.

Unauzungumziaje umri katika kukusaidia au kukuangusha?!!

Umri hakuwa kigezo hata kidogo nadhan ni sera zangu, kujiamini kwangu na kutokuwa na uoga wakutetea kile ninachoona nina haki nacho bila kuvunja sheria

Tayari tukiwa tumemaliza mwaka sasa tangu serikali ya awamu yanne iingie madarakani na Amina akiwa mmoja wa wanaounda serikali hii kama mbunge wa vijana kwa tiketi ya chama tawala tayari ameshaonyesha uchapaji kazi ambapo ameshaanzisha kombe la vijana ambalo ameliita Bongo Cup ambapo vijana kutoka kila mkoa wanaunda timu na kushindania kombe hilo ambapo.....kupitia kombe hilo vijana kadhaa watapata ajira kwani vipaji vyao vitaonekana na kusajiliwa kama si kuuzwa nje ya nchi kwenye timu kuubwa duniani

Mbali ya Kombe hilo Amina ameanzisha vita juu ya madawa ya kulevya bungeni ambapo amejitolea kufa na kupona ili madaya ya kulevya ambayo yamekuwa kikwazo katika maendeleo ya vijana ambao ndio waathirika wakubwa kupigania madawa hayo yakomeshwe ambapo amejitolea kushirikiana na polisi kwa hali na mali......na yote hiyo ni katika kugombea maslahi ya vijana ambao ndio taifa la leo

madawa ya kulevya inanisikitisha saana na ndio nimeianzisha bungeni ili wafanye juu chini kupambana nao hao wanaoyaingiza nchini.

...ningeomba sheria za madaewa wa kulevya yabadilishwe...mfano mtu akibaka anapewa kihukumu ya kifungo cha maisha...lakini muuza madawa ambaye anawaumiza vijana kibao analipishwa pesa chache na kuachiwa.

nawashangaa watz.....wanadai ninatafuta umaarufu upi kwanini leo wakati mi nilikuwa maarufu kabla sijaingia bungeni na ndio maana wengine walihoji kuwa nimepewa ubunge kwa vile mie kimaarufu...wanasahau mie ni mbunge na natimiza majukumu yangu

madawa ya kulevya yaathiri vijana tutakuwa na taifa gani sasa kama vijana kibao wanaathirika na madawa ya kulevya? alihoji amina

Mr & Mrs Mpakanjia

Ushauri kama mbunge mwanamke

kuwashauri wanawake...wajitokejeze kupiga kura wawachague viongozi wanaowafaaa, nawagombeee nafasi tofauti, ikiwezpo katika vikundi majumba, makazini na serikalini pia


tusiwaache wanaume pekee yao nasi tunaweza tuudhihirishie jamii kuwa wanawake nao wanaweza yaani wakisimama wawili watu wasione tofauti.

Amina pia alisisitizia umuhimu kwa vijana na siasa
Lazima maana sie kama vijana ndio tujuao matatizo yetu,,,wazee hawajui mfano waathirika wa madawa ni vijana sio wazee...hakuna wa kutusemea ni sie wenyewe tunahitajika tuje kuelezea yanayotukabili
na waamini wanaweza sio ngumu,,,waache uoga

Ni hayo tu kuhusu Amina una swali?!!


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.