Sasa ni safari kuelekea Hollywood!!
Nimekuwa wakwanza kuingia Nollywood,naomba mungu anisaidie na niwe wakwanza kuingia Hollywood Hayo maneno ya muigizaji na mtunzi wafilamu nchini maarufu kwajina la Steven Charles Kanumba maarufu sana kama kanumba pindi alipopata wasaa wakuzungumza na Darhotwire..
Baada yakusakanyana saana na Kanumba hatimaye tulikutana na Kanumba maeneo ya \'migo Migo\' Magomeni katika ukumbi wa Lango lajiji, maskani yao makuu wasanii wakundi la Kaole
Kama ilivyo ada tuliomb kanumba atupe jina kamili na historia yake kwa ujumla\\
....Naitwa Steven Charles Kanumba,nilizaliwa mkoani Shinganya Januari 8 ,1984
na kuanza elimu yangu ya msingi katika shule ya Msingi Bugoyi,na kishakuingia katika sekondari ya Mwadui ambapo sikumalizia hapo nilipofika kidato cha pili nikahamia katika shule ya Dar Christian Seminary nilipomalizia elimu yangu ya kidato cha nne na kujiunga na shule ya Sekondari ya Jitegemee ambapo nilisoma kidato cha tato nasita....alijielezea Kanumba
Aliezea historia yake kisanaa ambako alisema tangu akiwa mdogo alipenda kuigiza kiasi kwamba kuna maneno mama yake humwambia aliwahi kumwambia kuwa alipokuwa mdogo kuna siku alishika mkanda wa filamu na kumwambia mama yake nikiwa mkubwa nataka nije kuigiza kama huyo.
Lakini safari yake rasmi katika sanaa aliianza mwaka 2002 ndani ya kundi la sanaa la Kaole ,baada ya kuzunguka katika makundi kadhaa bila yakupata mafanikio hadi alipotua kaole ambapo alianza kuigiza mchezo wa Jahazi ambapo aliigiza sehemu tu ya igizo hilo ambapo iliitwa ishu ya 500.
Igizo lake la pili lilikuwa Dira ambapo aliigiza kama mchumba wa Dida ambapo wao walipendana wakiwa mjini kumbe huko kijijini wazazi wao ni chui na paka.
Igizo lake la tatu ambalo aliigiza lilikuwa ni Zizimo ambalo aliigiza kama kaka yake Kemy
Baada ya igizo hilo kuisha na ye kuwa ameigiza maigizo manne ndipo alipoingia rasmi kwenye utunzi ambapo alitunga igizo la Tufani ambapo ndio hii filamu iliyobatizwa jina la Johari .....kama mfuatiliaji wa filamu lazima umeshaiskia kama si kuiona.
Baada ya Tufani kuisha akaigiza igizo la Gharika ambapo aliigiza kama mdogo wa Frank ambao waliachiwa mali za urithi lakini kaka yake akawa anajirusha kwa saana na vimwana
na baada ya igizo hilo mkataba na kituo cha ITV , Luninga waliyokuwa wanarushia maigizo yao ulisha na wao kuhamia katika luninga ya TVT
.......Hadi kuhama ITV ni mambo tofauti yalitokea mbapo uongozi wa kikundi cha kaole pia ulibadilika na ndipo tulipoanza na kurusha igizo la Baragumu ambalo linaendelea hadi sasa ukiwa ni utunzi wangu pia.....alitanabaisha Kanumba
Wakati wanamalizana mkataba wa ITV tayari walikuwa na filamu yake ya kwanza aliyoita jina la JOHARI ambapo iliratibiwa na kampuni ya Game 1st Quality na ndipo alipokuja na filamu nyengine ya Sikitiko Langu, Johari 2, Danderous Desire na sasa ni Dar to Lagos ambayo inatimiza idadi ya filamu 7 alizotunga na kuigiza.
Tukiizungumzia hii filamu ya Dar to Lagos ambayo imemtoa...kwani ameigizia nchini Nigeria...pamoja na waigizaji wa kinigeria na ni utunzi wake na ndio filamu ya kwanza iliyozinduliwa Tangu ameanza kuigiza filamu.
Aliingiaje Nigeria (NOLLYWOOD) Nchi ambayo inasifika katika uingizaji wa filamu ukiwatoa waingereza,Marekani na wahindi.
Nilikuwa na malengo yangu tangu enzi hizo nilimwambia mkurugenzi wangu Mtitu Game, ambapo katika safari zake alibeba cv yangu pamoja na kazi zangu nilizokweshakufanya nakupeleka Nollywood Nigeria ambako alipowaonyesha walinikubali na wakaniita kwa ajili ya interview ambako nilifanya interew na nikapita na nilihojiwa na MNET ya Afrika ya kusini
......Na baada ya jamaa kunikubali ndipo nikaaanza na kazi ya kuigiza hii kazi ya DAR 2 LAGOS.
Nilitaka kujua wanigeria wasiojua kiswahili hata cha salam aliwaconvince vipi hadi wakakubali kuigiza filamu ambayo inalugha ya kiswahili....ukizingatia mtunzi (Kanumba ni mchanga katika fani)
......aaaaa!! dada ndio tofauti yetu sisi wasanii watanzania na wale wa Nigeria...wale kila siku wanataka wafanye kitu kipya,.....tena waliipenda saana baada ya kusoma hadithi na kuona ilivyo nzuri walikubali kufanya...tena kiswahili ndio kilichowasukuma zaidi.....kwani walidai kila siku wamekuwa wanaigiza kwa kiingereza hivyo hii kiswahili imewaongezea chachu katika CV zao.
Ndo kama hivyo wakakubali kufanya hii movie kama unavyoiona ambapo kampuni ya Game 1st Quality ilipofanyakazi yake ya kwanza ndani ya Nollywood chini ya Director mkali Femi na wasanii Mercy Johnson na Bimbo Akintola na Nancy Okeke uzinduzi ulifanyika Diamond.
Baada ya hiyo movie tayari nishapata kazi kibao ambapo nitazifanya hapa nchini na baadae nitaenda nchini Nigeria kwa ajili ya kazi nyenginezo ambazo zikitoka mtasisikia
Nilitaka kumjua mtu anayemkubali katika sanaa alinitajia muigizaji kutoka Nigeria Olu Jacob, na alimtaja Eddie Murphy kutoka majuu huku hapa nyumbani akimtaja msanii wa kike Mainda.
Nilipenda kujua mafanikio yake ni yepi ?
aaaaa!! mafanikio nayaona dada angu ndo kama hivyo nina kagari haka ambako kananisaidia kurahishisha shughuli za hapa mjini ...RAV 4, pia ninaisaidia kuintunza familia yangu....hivyo si haba......alisema kanumba huku akimwaga smile kama anaigiza.
Tayari kanumba ameshapata tuzo 'award' kutoka kwa Gazeti la Burudani la Babkubwa kama msanii bora wa 2006 -2007
Kutokana na mafanikio hayo Kanumba ana matarajio tayari ambako anampango wa kurudi shule kusomea masuala haya haya ya uigizaji, ili aje kuwa BIG STAR....nimeandika kwa herufi kubwa kuweka msisitizo kama ye alivyotamka......na anawish aje kuingia Hollywood ndipo alipojipa moyo kuwa kama alikuwa wa kwanza kuingia Nollywood basi hata Hollywood atawaongoza pia.
Kanumba ni mzalendo wa haja kwani anadai ile kuwazungumzisha wanigeria kiswahili ni uzalendo tu wa nchi yake hivyo ataendelea kuitangaza Tanzania na kukitangaza kiswahili kwa ujumla.
Mbali ya matarajio pamoja na mafanikio aliyoyapata pia Kanumba alielezea vikwanzo anavyokutana navyo katika sanaa hii ambapo alianza na pirates(wezi wa kazi zao) haawa sio siri ndio kikwanzo kikubwa kinachotukabili sisi kwani wanatulostisha...kila siku tunalia
Kingine aliitaja serikali....serikali bado haitaki kututambua sisi...hapo namzungumzia msanii hathaminiwi kiivyo wakati wasanii wana nguvu saana katika jamii. hivyo tupewe nafasi na tuthamiiwe sawa na nguvu ya kazi yetu
Pia aliuelezea uzalendo..aiseee sie watanzania sio wazalendo...mtu yuko radhi kuthamini vya watu kushinda kazi za hapa nyumbani....ukilinganisha na wanigeria sie watanzania tunabidi tuwe wazalendo wakusapotiana sisi kwa sisi.
Chamwisho ni sisiwenyewe wasanii, tuna ile kurudishana nyuma mtu unampa kazi unamueleza hali halisi kulingana na Game ye anaanza kudai pesa nyiingi ili kukukomoa...tunakuwa tunazidi kudidimia sisi kwa sisi na matokeo yake ni fani kufa.
Kwa kumaliza Kanumba alitoa ushauri kwa wale ambao wanaona wana kipaji na wanataka wawe waigizaji.......mi nawashauri wasiibeeep sanaa, yaani sio waje kuigiza sababu wanataka umaarufu, au sababu wameona fulani amefanikiwa...bali wawe tayari kufanya kazi hata kwa kujitolea
Na pia aliishauri serikali itambue uwepo wao....Mfano Nigeria wamefanikiwa kuinda Nollywood sababu ya kusapotiwa na serikali yao....mimi naamini tunauwezo hata kushinda wanigeria iwapo tutapatiwa nafasi.
Na alimaliza kwa kusema serikali ielewe kuwa msanii anaweza iharibu au iendeza jamii kwa 99%....angalia misiba, vita, sherehe wasanii ndio wanaoelimisha jamii.
Kanumba alimaliza kwa kutoa shukran zake za dhati kwa Mama Yake mzazi,mkurugenzi wake Mtitu Game,kundi la Kaole pamoja na Ckriss Mhenga pamoja nawooote waliomfikisha hapa alipo.
Na kwa mawasiliano zaidi na kanumba cheki nae kwenye stevekanumba@yahoo.com

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala