Juda kuwatoa mamodel wa kiBongo!!
kuitoa Bongo???Hapa nazungumzia makampuni yote watumie wanamitindo wa kitanzania ambao kampuni wa Juda wanawaandaa na hata watoke nje ya nchi kwa ajili ya kufanya matangazo hukooo
Watu ukiwaambia bongo sasa hivi ni New York wanabisha,sasa hebu ona mambo makubwa ya kiulaya ulaya wanayofanywa Juda Modeling and Casting Co Ltd.
Diana Mhere
Ilizoeleka kama una harusi yako na unatafuta wasichana wa kuvutia kama wasimamizi, lazima ukamchuke mtoto wa shangazi. Hii ilikuwa inaleta mushkeri kidogo maana wengine wanakuwa wanapishana vimo na mambo kama hayo.
Sasa huna haja ya kwenda kwa shangazi ni kiasi cha kuwaona juda, wao wana Wasichana maalumu kwa ajili ya kazi kama hizo.
Kwa wasanii pale unapotaka kupiga picha za video , sasa siyo tena wakati wa kwenda kutafuta poda za sh 250 na kuwazoa watu wa mtaaani kwenuna kuwafanya wahahe kuazima nguo, kwanijudah watakupatia watu wao kusherehesha na kupendezesha video yako.
Lakini kubwa zaidi ambalo wanafanya ni kutafuta model’s na mtu yeyote ambao wao wanaonaa atawafaa katika kupiga picha za matangazo,iwe ya video,au bango,au gazeti.
Kivipi basi utanufaika na juda pindi watapotumia picha yako,anasema Diana Mhele mkurugenzi wa Juda Models Company.
”Kama wewe unaona unashepu kiuanamitindo, unafaa kwenye tangazo lolote basi au kuonyesha mavazi unaweza ukafanya mawasilano na sisi na tukaweza kuongea zaidi,ila pia sisi tunatembea kutafuta watu kutegemea na aina ya watu ambao tunawahitaji,haijalishi kama ni mwanamitindo au mrembo mzww au mtoto”.
Anasisitiza baada ya kuingia mkataba na muhusika,na pindi picha yako itakapotumia watakupatia mapene(hela)yako na tayari utakuwa umetengeneza ”shavu”. Ila kwa kipindi cha mkatabata utaweza kufanya kazi zako zingine kama kawa ila si katika kampuni inayofanya kazi kama wao.
Kwa wale wa mikoani kaeni mkao wa ”kula kwenye shughuli” kwani juda wanaprogram ya kutembea nchi nzima kutafuta visura na watu wanaovutia katika kutengeneza matangazo na fashion show.
Lakini nani huyu basi anayefanya mambo yote haya makubwa? anaelezea hapa historia yake kwa ufupi yeye mwenyewe Diana Maisa Mhere,mkurugenzi wa Judah Models Company.
”Nilizaliwa miaka ya 80,Musoma nikiwa mtoto wa kwanza katika ya watoto wa nne wa marehemu mzee Mhele, nimesoma shule mbali mbali Arusha, Nairobi na Uganda, na baadaye nikaenda Uingereza kwa ajili ya kuchukua diploma ya Microsoft Engeneering.
Kabla ya kwenda Uingereza mwaka 1998
nilishiriki mashindano la kumsaka Miss Tanzania ambako nilianzia kwenye Miss Ilala na nikashinda taji la Miss Ilala na kupata tiketi ya Miss Tanzania ambako niliibuka mshindi wa pili.
Na niliwahi kufanya tangazo la TTCL mwaka 1998 na pia nilikuwa model katika kampuni ya Faces International
Nilijaribu kumuuliza Diana ilikuaje akapata wazo kama hili ambalo linaonekana ni geni katika nchi yetu, na anahakikishaje anakuwa juu hata pale baada ya wabongo kuiga,manaa sisi ni hodari wakusubiri flani aanzishe tuige.
Nikataka kujua je Diana ujuzi huu aliupata wapi labda kama aliuendea shule au la
....hapana sikusomea shule ila nilivyoamua kuaingia katika hii field nilikuwa nasoma saana vitabu na kushinda kwenye internet kusoma ni nini kinatakiwa na kusikiliza ushauri wa watu ambaop wanajua hii kitu....
Anasema ”nilikuwa Uingereza na nilienda katika studio moja ya kupiga picha baada ya kupiga picha, yule jamaa wa studio aliniambia kuwa navutia, na anaweza kiutumia picha yangu katika kutafuta watu wataotaka matangazo
Baadhi ya mamodel wa Juda
Nilifanikiwa kupiga picha ambazo walizitumia katika Gloss Magazine mwaka 2002 kabla ya kurudi hapa bongo.Baada ya msiba wa baba yangu.
Kwa kuwa mimi ndiyo mtoto mkubwa kwetu nikaona badala ya kusafiri nje ni bora nikae kuangalia wadogo zangu na baadhi ya miradi aliyoiacha marehemu baba.
Sasa hapo ndipo nikaona kwa kuwa nimeamua maisha yangu yawe hapa basi naweza kufanya yale mambo ambayo nilikuwa na ndoto ya kuyafanya huko ugenini.(nje)nashukuru mungu nimeanza vizuri na mafanikoi ninayaona japo si makubwa sana”
Kama Juda tumeshafanya kazi na kampuni nyingi nchini ambao tuliwapa wanamitindo wetu ambao walitumika katika matangazo mfano ya FCB tangazo la sms , ZK tangazo la TTCL,CRDB Bank, Zantel,Scanad katika tangazo la kampain ya Tigo, Matumaini na Fashion show ya Twiga Cement.
Diana alizungumzia vikwazo wanavyokutana navyo katika hii kazi kuwa ni pamoja na kumfuata mtu especial wasichana na kuwaambia unataka wawe wanamitindo , wanakataa na kusema mie sitaki kuwa miss
lengine ni kampuni fake za modeling hapa nchini maana unasikia mtu ana kampuni ya Modeling unamuuliza imasajiliwa anabaki kutoka macho....na hao ndo wanafanya hii kazi iwe ngumu maana wao wanapelekewa model kwenye kampuni za matangazo kwa bei ya chini na hawafuati sheria kiasi kwamba sie wenye leseni ya hii kazi tunaonekana tuko juu.
Matarajio ya Diana ni kuja kumtoa mrembo ambaye ataiwakilisha nchi katika shindano la Face of Afrika na kuitoa Tanzania kimaso maso
Ndo maana nimepanga kutoka nje ya Dar es Salam ambako nitaenda kusaka wanamitindo ambapo wakti wakija watu wa Faces nipeleke model kyutoka Juda ambapo wakaguzi kutoka Afrika kusini watachanganyikiwa washinde jua wachukue yupi na waache yupi ...usishangae ukisia wasichana 17 wote wametoka Tanzaia kwani wote watakuwa na vigezo....alijifagilia Diana huku akiachia tabasamu.
...kunakuwa kuna tatizo la watu kutofautisha umiss na uanamitindo..... japokuwa siku zinavyozidi kwenda tunashukuru tunaona mabadiliko watu wanaelewa....ukizingatia mie ninaowasaka saana ni wanafunzi hivyo wakimuona mwenzao katokea kwenye tangazo wanakuwa wanaelewa ni nini nafanya haswaa ukiwaambia kuwa watalipwa pia...alisisitiza Diana.
Mwisho Diana ana wataja na kuwashukuru watu ambao kwa namna moja au nyingine wamemfanya yeye awe hapa”mama na marehemu baba yangu,mkurugenzi wa DTV na Photopoint na wote wanaonipa sapoti nasema nawapenda sana”.alimaliza Diana

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala