Tafuta DHWTangazaTuandikie
Mbunifu aliyeiendea shule fani!!

Nasikitika kuona Tanzania inakuwa dampo la takataka za nguo za mitumba wakati tuna uwezo wa kulima pamba na kutengeneza vitambaa safi vya pamba na kubuni mitindo tunayoitaka ” ndivyo anavyoanza kusema Mbunifu wa Mitindo Ailinda Sawe
alipofanya mahojiano na Darhotwire.

Anaendelea kusema,” Mimi kama mbunifu na wa mitindo mkongwe nchini nitahakikisha kwanza nchi ya Tanzania inatambulika sio tu kwa bendera bali pia kwa vazi maalum ambalo kwa umahiri tulionao wabunifu wa mavazi Tanzania naaminika tutafanikiwa katika hili,”


Ailinda Sawe

Akielezea dhamira yake ya kuitangaza Tanzania anasema amedhamiria kutumia vazi la kanga ili kutangaza nchi yake kwani ni vazi linalovaliwa sana.

”Nipo katika mkakati wa kubuni vazi hilo na tayari nimekwishaanza maandalizi kwa kuchora pamoja na maandalizi mengine na baada ya muda mfupi litakamilika,”anasema.

Mbunifu huyo anasema ameshiriki katika maonyesho hayo ili kuionyesha jamii kuwa Mtanzania ana utambulisho wake hasa kutokana na mavazi mbalimbali ya Kitanzania aliyoyabuni maalum kwa ajili ya maonyesho hayo .

Mwanamama huyo anasema amezaliwa mwanzoni miaka ya 50 katika wilaya ya Machame, Nronga na ni mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro. Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi
Nronga kati ya mwaka 1959 na 1965 na elimu ya sekondari katika shute ya sekondari Machame Girls iliyopo katika mkoa huohuo kati ya mwaka 1966 na 1969 Baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari alijiunga na Chuo cha Civil Service Training College kwa ajili ya kuchukua kozi ya uhazili.

Hata hivyo hakuipenda taaluma hiyo na hivyo aliamua kuachana nayo mwaka mmoja baadaye na kujiunga na Chuo cha Ardhi.

Alisoma katika chuo hicho kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kuitwa na Umoja wa wa wanawake wa kikristo(YWCA). Kuitwa kwake huko kulitokana na juhudi za umoja huo kupitia katika shule za ufundi na kuchagua wale Waliofaulu vizuri.

Kutokana na programu hiyo, YWCA ilipata taarifa ya Ailinda kuwa ndiye mwanafunzi aliyefaulu vizuri kuliko wengine na hivyo
wakamuita kujiunga na umoja huo Mwezi mmoja baada ya kujiunga na YWCA walifanya mtihani na yeye alifaulu vizuri peke yake na kupata nafasi ya kwenda kusoma nchini ’Ugiriki mwaka 1971.

Akiwa nchini Ugiriki alijiunga’.na chuo kimoja cha YWCA katika mji mkuu wa nchl triyo Athens kwa kozi ya mwaka mmoja ya sanaa na ubunifu wa mitindo.

Mwaka 1972 alihitimu na kurudi nyumbani Tanzania kwa
ajili ya ujenzi wa taifa .Baada ya kurudi nyumbani aliendelea na kazi yake YWCA hadi kufikia mwaka 1979 alipopata nafasi nyingine ya
kwenda kusoma nchini Uingereza.

Ailinda alisema kozi Uingereza ilikuwa ya miaka mitatu na nusu na ilikuwa ya teknolojia ya ubunifu na nguo ambapo baada ya kumaliza alifanikiwa kupata Stashahada ya Juu.

”Nilipomaliza tu kozi yangu mwaka 1983 huko Manchester, mwalimu wangu alinitafutia sehemu kufanya kazi lakini sikuona sababu ya kueneza ujuzi wangu katika nchi ya ugenini wakati taifa langu linanihitaji,”anasema.

Akifafanua kilichomvutia kurudi nchini mara baada ya masomo yake anasema,...
....”nina mapenzi makubwa na nchi yangu ya Tanzania...nina hamu kubwa ya kuona ujuzi wangu unarithiwa na vijana katika taifa langu
kwa manufaa ya taifa na si vinginevyo.....”

Ailinda alirudi nchini mwaka 1983 na kuendelea na kazi yake YWCA hadi mwaka 1988 alipoamua kuanzisha kampuni yake binafsi inayojulikana kama A.S Designs.

Akielezea mafanikio yake katika fani ya mitindo anasema alishawahi kuwa mratibu wa tamasha kubwa la mtu mweusi lililofanyika nchini Nigeria mwaka

1977 lililojulikana kama ”The 2nd world black and affg festival of arts and culture.”

Mafanikio mengine ni kukubalika kwa vazi lake la ubunifu nchini na nje ya nchi.

Mavazi yaliyotengenezwa na Ailinda kupitia kampuni yake ya Afrika Sana

Anasema vazi hila lilikuwa ni la asili ya kabila wamasai ambao hufunga rubega lakini amelisuka na kufanya livutie zaidi

Ailinda anasema pia amebuni vazi la morani kwa wanaume ambapo lilishika nafasi ya pili kitaifa mwaka jana.

Mwanamame huyu pia anasema mafanikio mengine kuweza kumudu kazi zake katika fani hii ya ubunifu wa mavazi na utengenezaji wa batiki.

”Mpaka sasa ninamiliki kampuni inayojulikana kama Afrika Sana , nikiwa na mumwe wangu pamoja na watoto wangu, kwa bahati nzuri watoto wetu ni wabunifu wazuri wa mavazi mbalimbali anaelezea mama huyu.

Anasema anafarijika sana kuona familia yake inalipa kipaumbele suala ubunifu wa mitindo na hasa ya kiasili kwani inahifadhi utamaduni wetu na pia wanautangaza kwa nguvu zote kama afanyavyo yeye (Ailinda).

Akisisitiza umuhimu wa kuyaenzi mavazi ya kiasili Ailinda anawashauri kinamama kuweka alama ya Kiafrika katika kila aina ya mavazi wanayoyavaa kila siku ili kuonyesha ni jinsi gani wanajali utamaduni wao.

Mbunifu huyu anasema ingawa watu wanahitaji nguo za aina mbalimbali bado suala la maonyesho ya mavazi katika jamii ya Watanzania ni geni.

Anasema kila siku jamii imekuwa ikiichukulia hii kwa mtazamo tofauti kwani wapo ambao wanaona fani hii kuwa ni ya kihuni yaanii wanaoshiriki katika fani hii ni watu wasioheshimu.

Ailinda anaendelea kusema kuwa pia wapo wengine wanaoiona kama ni mambo ya kuiga kwa mataifa makubwa hasa ya Magharibi bila kujali kuwa utamaduni wetu unahitaji kutangazwa hasa ndani na nje ya nchi yetu

Na hii itatusaidia kuwa na hazina ya kutosha na pia kushindana katika fani,hii ya mavazi hasa kwa kutohoa aina fulani ya mavazi kutoka katika mitindo fulani na kuhamishia katika mitindo mingine ili kwenda na wakati.

mamahuyu.Ana ujumbe kama si wito kwa wanamitindo wachanga wawe wabunifu wa villi endelevu na bila kusahau asili yetu.Wasipende kuiga kwani kwa kufanya hivyo watakuwa tegemezi wa vitu vya nje.

.Waelewe pia vitu vilivyosanifiwa Kitanzania ni utambulisho wetu hivyo ni muhimu kuvipa kipaumbele.

Anasema vijana ndio taifa Ia Leo na baadaye na kwamba wanategemewa sana wabunifu wachanga kwani vichwa vyao bado vinafanya kazi na kuwafanya kuwa wepesi kubuni mambo mazuri zaidi.





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.