Tafuta DHWTangazaTuandikie
Ungaro ungaro saa za mchana wa jua kali




Fashion hizi zitatufanya tuonekane machizi

Miaka ya karibuni ulikua ukionekana umetinga mavazi yenye urembo wa kung’aa au meremeta wakati wa mchana ulikua unaonekana mshamba wa kuja.

Tofauti na siku hizi ukitinga kivazi chenye urembo wa kung’aa unaonekana mjanja tena unaenda na wakati.

Kama kawa wanamitindo wanahamasisha kuzalisha bidhaa zenye ungaro hususani wa silver na gold.

Usishangae ukiwa unakatiza mitaa ya posta ukapishana na mdada katinga kipochi au kavaa viatu vyenye rangi ya dhahabu au fedha na mkanda kiunoni ili kubalance (kumechisha).

Utaona top ”blauzi” au bazee limedariziwa kwa urembo wa dhahabu pamoja na fedha.

Ili kuungana na wajanja usisite kuinunua ukipishana nayo wakati wa shopping.

Its all about styles!!


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.