Kama unayo usitupe Shost!!
Jamani zile PAMBA walizovaa bibi zetu enzi hizoooo zimerudi tena upyaa japokuwa zimenakshiwa kidogo na wamebadilisha majina.
Gypsy a.k.a Charanga ama Sinderela ukipenda na wedge sole, kazi kwenu Mashost
katika pita pita zangu za hapa na pale na kuperuzi mitandaoni katika tovuti za madesigner maarufu duniani nikakutana na hizi sket mpya wenyewe wamezipachika jina la GYPSY , japokuwa hapa kwetu wanaziita SINDERELA na enzi zile mie bado msichana walikuwa wanaziita MACHARANGA.
Si hizo sket tu bali kuna viatu pia ambavyo ndo vinatesa katika masoko ya mitindo navyo wenyewe wamevibatiza jina la WEDGE SOLE wakati enzi zileeeee viatu hv nilisikiwa vilikuwa vinaitwa MADIGANZA AU SHUKA TUBONGE, wasichana wa miaka ile nitakuwa naongea nao lugha moja.
Sasa jamani wenzangu warembo wa leo hii ndo nawasisitizia kama mnavyo msivitupe yaani vile vitu vyooote walivyovaa mama zetu na bibi zetu enzi zileeee ndo vinarudi upyaaa angalia style za hereni, viatu na hata nguo hivyo msivitupe watunzieni wajukuu na vitukuu zenu watakuja kutesea huko mbeleni.....cheers
 |

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala