Mapambo ya miaka ileee haya hapa!!
kweli waliosema ya kale hayanuki hawakukosea, leo hii mie nimetinga mapambo aliyovaa bibi yangu enzi zileee!! mwenyewe akiniona anatabasamu tu!!
ni kuhusiana na hizi bangili na chain pamoja na hereni ’Accessories’ kama wanavyoiita wenzetu zilizongia sasa ambazo kina dada na macelebrate kibao wanalipuka nazo
ni hereni kuubwa na ndefu, pamoja na mabangilia mapanaa ambayo yanakuwa na rangi tofauti au rangi ya shaba kama si fedha na pamoja na chain ambazo zina miundo ya duara na maumbo tofauti na zinakuwa na urefu ambapo unaizungushia shingoni kutokana na mtindo wa nguo uliyovaa
zipo katika material tofauti, chuma, plastic na magome ya mimea pamoja na madini tofauti tofauti.
Ndio utavaa nguo yako na kiatu bomba bila kutupia ka
’Accessories’ hata kidogo wajanja wataona umepwaya tu....
hivyo bi shost visake basi Naomba niwape tipu....’KUMECHISHA SASA BASI’ mambo yale unamechisha kuanzia kibanio cha nywele . pochi viatu na nguo mwisho
unaweza vaa rangi tofauti ila zinazoendana hata ukichotea ’Accessories’ na make up inatosha!!
 |

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala