Huyo ndo Wema Sepetu!!
Miss Tanzania 2006, aliyezaliwa mwaka 1988 tarehe 28 mwezi wa Septemba ndani ya jiji la Makamba ...mh!! samahanini sikuhizi Kandoro.
Jina lake halisi ni Wema Sepetu hakuna a.k.a kwenye umiss Jamani msijentolea macho mbona sijataja mkajua ni mwanamuziki huyu ni Miss
Wema Sepetu
Wema ambaye nilikutana nae katika Ofisi za Miss Tanzania akiwa katika harakati za kujiandaa na safari yake kuelekea nchini Poland ambako anaenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kumsaka mrembo wa dunia 2006 .
Wema akiongea kwa kujiamini alisema yeye ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wa nne wa Mzee Sepetu
Anasema Elimu yake ya msingi hadi sekondari ameipatia katika shule ya Academic International iliyopo maeneo ya Mikocheni ,Dar es Salam
...Ndio nimemaliza kidato cha nne nikiwa nasubiria kwenda college nchini Canada ambako ntasomea mambo ya Finance.
...lakini kwanza nataka niutumikie huu mwaka wangu kama Miss Tanzania na nikimaliza ndio nitaendelea na masomo cos education is always there huu umiss unapita tu.....aliongezea Wema.
Akizungumzia hii fani ya urembo Wema anasema amekuwa akiitamani siku nyingi kushiriki ila alikuwa hajajua pa kuanzia hadi mwaka huu alipofuatwa na muandaaji wakitongoji cha Upanga akimwambia ashiriki Miss Upanga
...huku akicheka Wema anakiri kusema alimkatalia huyo jamaa na kumwambia aka mi sihitaji kushiriki Miss Upanga huku akiwaza ye anapenda kushiriki Miss Tanzania tu
...jumapili moja nikiwa slip way nilikutana tena na muandaaji wa Kitongoji cha Miss Dar Indian Ocean, Mange Kimambi ambaye aliniafuata na kuniambia nishiriki kitongoji chake..... nae alimjibu kuwa ye hataki kushiriki Miss hizo ye target yake ni miss Tanzania
Anasema Mange alifanya kazi ya ziada ya kumweleza kuwa Miss Tanzania inaanzia vitongojini ndipo akasema ohoo!! poa wacha niongee na familia yangu, ndipo alipoongea na dada yake na wazazi wakampa baraka zote na ye kuanza mazoezi katika kitongoji Dar Indian Ocean hivyo ndivyo safari ya Umiss ilipoanza
Kama ilivyo ada kwenye mashindano lazima mshindi apatikane,Wema Sepetu katika kitongoji bahati haikuwa yake pale alipopigwa kikumbo na Mrembo Nadia Mohamed ambaye alishika nafasi ya kwanza na yeye kushika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikiwa imebaki kwa mrembo Vivian Sirikwa.
Wema anakiri kuwa alichemsha katika kujibu swali katika shindano la Kitongoji kutokana na kutokuwa na uzoefu na mashindano hayo lakini akawa amepata tiketi ya kushiriki Miss Kinondoni ambako alipania kufukia mashimo yote ambayo aliyaacha katika Miss Kitongoji.
......Sio siri niliamini ningeshinda Miss Kinondoni sababu nilishajua makosa hivyo nilijitahidi kujiandaa lakini hadi leo hii siwezi kujua kwanini sikushinda na sio siri nilikata tamaa kabisa maana sikuwa nimejiandaa kushindwa hadi mama angu akaniambia wala usikate tamaa mradi maji umeyashavulia nguo huna budi kuyaoga...hivyo nilienda Miss Tanzania kushiriki tu katika kutimiza wajibu tofauti na Miss Kinondoni ambako nilijiandaa kushinda tu....alisema Wema
Kama Zali Wema ambaye alikuwa ameshakata tamaa na yupo tayari kwa lolote ambalo lingetokea usiku ule ndo alitangazwa kuwa Miss Tanzania 2006
Akielezea kambi ilikuwa mwake na ndio iliyompa ujasiri wa kufanya maajabu usiku wa tarehe 5 mwezi wa nane siku ambayo historia ya maisha yake ilibadilika
Wema kama Miss Tanzania ambaye analo linalomsubiria anasema, yupo anajiandaa na shindano la Miss World ambalo litafanyika nchini Poland mwezi ujao
...Sitaki kuahidi chochote ila nasema nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kwani najua nimeibeba Tanzania kwenye hili lakusaidiwa ni sala na maombi ya watanzania tu....alisema Wema
moja kati ya kigezo kilichomshindisha Nancy ilikuwa ni kipaji nilitaka kujua,Je Wema ana kipaji gani??
....mi ninavipaji luluki, naweza cheza basket ball,naogelea,naweza kubelle dabce (mauno) na soka nacheza, hivyo usiwe na shaka juu ya hilo...alinijibu Wema huku akijishebedua
Zaidi as hobby Wema anapenda saana kusoma vitabu
Matarajio ya Wema anasema huu mwaka ataudedicate kwa taji hili la Miss Tanzania ambako na shule kaahirisha kwenda ili tu aweze kufanya kazi za kijamii kama ilivyo ’moto’ wa taji hilo
.....Hoyce Temu ndio role model wangu hivyo nitajitahidi kufuata nyayo zake na kwa msaada wake yeye pia nadhani ntaitumikia jamii kama yeye alivyofanya tangu alipotwaa taji mwaka 1999 hadi leo hii, sio siri ananihamasishaa....alinena Wema
Akiangalia mbeleni baada ya shule
Wema anapendelea kuja kuwa Finance Admin.....hiyo mtanisaidia kutafsiri
Wema anasema Exponsure ni moja kati ya mafanikio aliyoyapata kwani anadai Wema wa sasa huwezi kumfananisha na yuleee wa mwezi wa 7,(kabla hajavikwa taji)
..Zaidi ya hiyo sasa nina gari , Pesa na marafiki .
Ushauri
Ushauri alianza kuutoa kwa wazazi ambao bado wanaamini fani hii ya urembo ni uhuni na kuomba waachane na hiyo dhana
...mi tangu nimeshiriki katika ngazi ya kitongoji sijaona kitu kama hicho kinachofanywa cha kihuni, na ningependa wazazi wasisikilize maneno ya mitaani...alisisitiza Wema
Wema pia alikuwa na ushauri kwa warembo wenzie mbao aliwaambia kuwa kama yupo anajiona anauwezo wa kushiriki ashiriki tu zaidi wajiamini wanaweza waamue na watafanikiwa.
Baada ya ushauri Wema alipata nafasi ya kutoa shukran kwa mungu, wazazi wake, waandaaji kuanzia kitongoji Mange kimambi,Kinondoni Rahma na Yussuf George pamoja na kamati ya Miss Tanzania kwa ujumla na watanzania woote wanaomtakia mafanikio

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala