Tafuta DHWTangazaTuandikie
Maya atambulisha fani Bongo!!

Naomba mnipe nafasi ya kuaandika haya ninayoamini kuwa fani ya MAKE UP ARTIST ni ngeni hapa nyumbani kwetu...Nazungumzia TZ, kwani hata kiswahili chake bado sijakitambua....na ninaamini aliyeitambulisha hii fani ni mwana dada Maya Yaneska Al-Said.


Maya Yaneska Al-Said.

Najua mpoa mnaoguna au kutoa macho lakini nikielezea utakubaliana na mie kwani Maya ndio make up artist ambaye amejitoa kufanya kazi hii kama biashara kiasi kwamba hata wengine wamejitokeza sababu wameona alaa kumbe nasi twatambulika

Nilimtembelea Maya ofini kwake ambako anafanyia shughuli hizi katika duka la D-Jungle ambapo piwa wanauza pamba original zenye chata zinazolekewa duniani, kama Puma, Diesel na nyenginezo.

Maya alianza kwa kuniambia historia yake ambapo alisema alizaliwa Macedonia na kusomea huko ambapo alisoma masuala ya utalii na mambo ya mitindo ambapo ndo hii fani ya Make up artist.

Na fani hii aliianza mwaka 1999 ambapo aliwaremba Miss Macedonia , na tayari ameshawaremba wanamitindo walioshiriki fashion Show na wanamuziki na waigizaji tofauti nchini kwao na Hapa nchini Tz.

Anasema mwaka 2004 ndo alitinga nchini , na anaipenda Tanzania sababu ana marafiki kibao na anapaona Tanzania kama nyumbani sababu anapapenda.

Akiongelea fani hii anasema tangu utotoni mwake alikuwa na kipaji ambacho ambacho alikiendeleza kwa kwenda shule na kukufanyika kazi hadi leo hii ambapo baada ya masomo alipeleka cheti chake katika kampuni ya vipodozi vya M.A.C ambapo walimpitisha kama mpodozi wao. nae hutumia vipodozi vya MAC ambavyo ni vipodozi maarufu duniani.

Nilitaka kujua ni vp aliweza kuanzisha fani hii ambayo ilikuwa adimu saana maana watanzania wengi tunaamini saloon ndio unapata kila huduma inayohusiana na urembo kuanzia nywele hadi unyayo


.......nilianza hii kazi nyumbani Macedonia na nilipofika hapa nikaendeleza ..... kama unavyoona kulikuwa hakuna wanaofanya hii kazi lakini sasa atlist wameanza kujitokeza taratibu ....alijibu Maya

Nilitaka kujua anaonaje mapokeo ya watu kuhusiana na hii fani yake alikuwa na haya ya kusema......wanawake sasa wamepata awareness tangu aanze hii kazi kiasi kwamba kila mtu anajua umuhimu wa vipodozi yaani nikama sheria ukitaka kuwa mzuri kila siku huna budi kuvaa vipodozi

Nini amefaidika nacho tangu umeanza hii kazi hapa nchini?
Anasema amefanikiwa kwa kupata akitakacho na kufanya kitu anachokipenda.

Kama mjuavyo hakuna barabara isiyo na kona Maya nae ana matatizo katika hii kazi yake ambapo anasema tatizo kubwa analokumbana nalo ni la watu kutojua vitu fake na original kitu kinachopelekea kazi yake kuonekana ni ya gharama sababu wamezoe fake ambavyo ni rahisi.

Nilitaka kujua vipi ushindani anaokumbana nao... anasema hakuna ushindani wa kihivyo japo inategemea kila mtu ana watu wanaokubali kazi zao nami pia nina wateja wangu hata hivyo siogopi ushindani ukizingatia kuwa nafanya kazi bora.

Mara nyngi kwenye matangazo ya Maya hutumia mac kama vipodozi anavyotumia, ndipo nikataka kujua je yeye anashare kwenye hiyo kampuni au wanamdhamini



..... alianza kwa kutabasam na hapana sina share alijibu huku akiachia tabasam....Mac natumia sababu ni vipodozi bora na mie ni make up artist wao walinipitisha baada ya kupeleka vyeti vyangu na kuwaonyesha kazi zangu. hivyo waliniruhusu kutumia MAC.

Mbali ya kufanya hii kazi Vile vile Maya ni Fashion Stylist ,ambaye anasema hana role model sababu ana style za kipekee.

Ushauri anaoutoa kwa watu ni kuwa wawe na furaha wataishi maisha marefu.

Maya alikuwa na wasaa wa kushukuru ambapo alianza kwa kumshukuru mume wake pamoja na familia kwa ushirikiano wao na muda wao pamoja na wafanyakazi wa D-Jungle kwa kuwa waaminifu na hodari.




 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.