Tafuta DHWTangazaTuandikie
Mtambue Genevieve wa Bongo!!

Naombeni tu mniruhusu nimuite Genevieve wa Bongo.....KWANI?!!! anafanana nae kiuigizaji na hata kiumbo kama sikosei, siwajua u cant see what i seee...nimeongeza kibbc kuonyesha msisitizo. teh! teh! teh!!



Anaitwa Hawa mkamba. ila kwa sasa ni Mrs Smedegaard kwani tayari amepata mwandani wake....hivyo wakora hamna nafasi kwake(Sorry to disappoint you)


Hawa msanii anayeigiza kwa hisia na kumgusa yeyote anayekodolea macho screen kuangalia moja ya filamu zake ambazo ameigiza...kwani kwenye kuliza atakuliza na kwa kukuchekesha utacheka na kwa kutabasamu utatabasamu hakika utashindwa ficha hisia zako.

Amezaliwa miaka 26 iliyopita katika jiji hili hili la Makamba na alisomea Arusha na kuhitimu elimu yake ya sekondari mkoani humo kabla ya kuja jijini na kwa sasa anaishi nchini Denmark ambako anaishi na mumewe Mr Smedegaard.

Akielezea uigizaji...anasema yeye hajawahi kwenda shule ya hii fani wala katika maisha yake alikuwa hajaota kuja kuigiza, ila aliingia katika fani hii baada ya kushawishiwa na marafiki na wadau wa fani hii kwa kuambiwa kuwa anaweza na kama haamini ajaribu

.....sio siri sikuwahi kuwaza kuigiza mie japokuwa nilikuwa napenda saana kuangalia filamu hasa hasa za Kinigeria haswa haswa muigizaji akiwa ni Genevieve Nnaji........alisema Hawa huku akimwaga Tabasamu lenye bashasha!!

Alimtaja Mohsin Dr Cheni kama mtu aliyeanza kumshawishi kuigiza hadi akaanza kufikiria na hadi alipoibuka katika filamu iliyoitwa MASAA 24 ambayo yeye aliigiza kama mshka uskani .

Kwa mwaka huu 2006 Hawa ameibuka tena katika filamu ya SANDRA ambapo ndani yake kadhihirisha kuwa yeye anatoka sambamba na Genevieve ila amenisikitisha kuwa kunimbia naweza ukawa ndio mwisho wa yeye kuigiza.

..........Pia ipo filamu nyengine inaitwa jina la WHY ME?!! nayo niliigiza muda tu ilisimamiwa na DR Cheni nadhani anaiandaa ili iingie sokoni hivyo mashabiki wangu watege sikio......Alitanabaisha Hawa .

Hawa amenisikitisha aliponiambia kwa movie hizo tatu ambazo ameigiza zinaweza kuwa ndio mwisho wa yeye kuigiza akiwa na sababu kuwa ...kahamisha makazi ambako sasa anaishi Denmark na hizo filamu nyingi aliigiza alipokuwa hapa nchini.

...Si unajua nipo mbali huku ila mungu akijaalia nikarudi kwa muda mrefu nikipata nafasi nitaigiza.........Inshaallllaw!!...kila la kheri safari uliyoianza ina mafanikio usiiua gafla!!

Hawa ambaye ni mtoto wa tatu kuzaliwa katika watoto sita wa mzee Mkamba anasema kabla hajajikita kwenye fani hii ya uigizaji alikuwa na anapenda saana kusoma na kusafiri na mwenyewe anasema Thanks God ndoto zake zimeanza kutiki kwani sasa hivi ndo hivyo yupo nchi za watu na anasoma.

Hawa ambaye hobby zake anapenda muziki hasa hasa live band haswa Twanga Pepeta na FM......(Sijui huko Denmark atazionea wapi tena teh teh) na anaona raha saana akiwa anacheza na watoto

Role Model wake ni muigizaji wa kike wa nchini Nigeria Genevieve Nanji.

Nilimuuliza Hawa yeye akiangalia miaka mitano ijayo atakuwa nani anafanya nini na wapi
...alikuwa na haya ya kujibu...Kwa miaka mitano kwa kweli inategemea na uhai.mungu ndio anaejua kuwa nitakuwa wapi na nitakuwa nafanya nini.Ila kama ingekuwa uwezo wangu ningependa kuwa pamoja na mume wangu na watoto wetu katika maisha ya raha.na pia ningependa kuwa na kazi nzuri na maisha mazuri.

Hawa alituelezea matarajio yake katika sanaa
........matarajio yangu mimi, endapo nitarudi kuishi Bongo nitakuwa msanii bora wa Bongo.nitajitahidi kufikia angalau kama wenzetu wa Nigeria.ila kwa sasa nipo mbali , ila iwapo nitarudi na muda ukawepo na filam ya kuigiza ikawepo nitafanya kazi kwani sanaa ipo damuni.

Hawa alikuwa na ushauri kwa waigizaji wenzie katika kuendelea hii fani ....
me nawashauri kuwa tuwe serious kwenye location.kwa kuwa nimeona mengi kwenye filam nilizocheza kwamba watu hatusomi screept pindi tu tunapopewa ila matokeo yake tunasoma tukiwa location.na filam inakuwa haikuchangamka kwa kuwa muda unakuwa hautoshi .................tunatakiwa tujitahidi na tuwe makini na nini tunachofanya.pia nawashauri wenzangu tuwe tunapenda kuangalia filam za wenzetu wanaigeria.wameendelea sana katika uigizaji na ndio maana filam zao zinalipa ......alimaliza Hawa

Hawa alikuwa na ushauri kwa vijana wenzie kuwa.....ushauri wangu kwa vijana wenzangu ni kwamba tujitume kila jinsia, tusingoje kusukumwa au kuletewa.tufanye kazi kwa bidii.

Hawa anaamini wapo walimsaidia hadi yeye kufikia mahala hapo ambapo alikuwa na hawa wakuwashukuru Dr cheni, Mtitu, C2C , Darhotwire na watu wote waliochangia maendeleo yake kwa namna moja au nyengine



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.