Sinta J-LO wa Bongo!!!!
Christine John Manongi ndio jina alilopewa na wazazi wake baada ya kuanza fani ya kuigiza alijulikana sana kama sinta lakini baada yakukubuhu katika fani alianza kujiita JLO akimaanisha Jennifer Lopez wa Tanzania.
anasema alizaliwa katika miaka ya 80 na kuanza elimu yake jijini Dar es Salaam ambapo alipitia shule ya Mbezi na Cambridge sekondari na kisha akajiunga na chuo cha uandishi wa Habari na Utangazi DSJ ambako alitunukiwa cheti cha Diploma.
Akielezea usanii anasema anadhani ana kipaji kwani hakurithi wala hakusomea kuigiza na kikundi chake cha kwanza kuigiza ni Kaole Sanaa Group ambapo alikuja kusimamaa baada ya kupata kazi ya kutangaza mbayo ilikuwa nje ya jiji la Dar es Salaam ambako ni makao makuu ya kundi hilo.
Sinta akielezea mahusiano yake ya kimapenzi na msanii wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature ambao ulizua mzozo hadi Nature kutunga nyimbo za Sitaki Demu na Inaniuma Sana katika album yake ya Ugali.
.....ah mi niliachana na Juma nature bila sababu lakini magazeti ya udaku kwa namna moja au nyengine yalichangia sana kututenganisha maana yalikuwa yananiandika sana habari za uzushi na kuhusu kuniimba mi nadhani ni katika kutaka kuongeza mauzo ya album na kwa dizain fulani imempush kichizi.... alisema Sinta huku akicheka
Na kwanini wewe tu uandikwe zaidi magazetini na hadi upelekee kutishia kujiua....ah mi wanasemaga sura yangu inauza yaani siku picha yangu tu ikiaappear kwenye gazeti linakuwa linanunuliwa sana ndio maana wanapenda kuniandika hata kwa story zao za kutunga sasa hii inapelekea wanakuwa wananiandika vitu ambavyo vinanichafulia jina kiasi kwamba vinaniaribia hata maisha yangu.
Sinta anamtaja J lo kama role model wake kwani anazimia sana pale anapoandikwa sana lakini yeye anazidi kusonga mbele na ukizingatia yeye Sinta ndie aliyetwaa tuzo ya msanii wa kike aliyeandikwa sana magazetini Mwaka 2004.
”Nina sababu kibao za kujifananisha na Jlo mfano yeye ni msanii wa kuigiza na mimi naigiza yeye super staa na mimi super staa wa Bongo , yeye anaandikwa sana na mie naandikwa na kuimba naweza pia ila sema sijaamua tu.
Kwa sasa hivi Sinta ameacha kuigiza luningani ila anaigiza katika filamu zaidi na hadi sasa tayari ameshaigiza katika filamu ya Siri ambako ameigiza kama Mchumba wa Banana Zhoro.
Mafanikio aliyokwisha yapata Sinta ni pamoja na kuwa maarufu ,ambapo ameweza kufanya biashara zake binafsi ambapo kwa sasa anamiliki gari dogo aina ya Corola Limited.
Anatarajia kwenda nchini Uganda kusoma masuala ya Mass Communication ambako anataka sana hapo baadae aje kuwa Public Relation Officer
Anawashauri wasanii wapendane na anawaambai wasichana wasiwe tegemezi bali wachakarike waweze jitegemee wenyewe .
Akijielezea yeye ni nani hasa anakwambia yeye ni msichana anaejiamini na hana matatizo tofauti na wanavyomuandika magazetini
Anatoa shukrani zake kwa kundi la Kaole Sanaa Group, Ruge , Mungu na Wazazi pamoja na marafiki zake ambao ni JD,Maiza na Diana.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala