Masofa na vitambaa vya kufuma ...wapi na wapi
Leo nimeona nihamie mambo ya nyumbani kwani tumeng\'ang\'ania saana vivazi au mnasemaje mashost. naongea na nyie sababu ninauhakika nyie ndo warembaji nyumba unapeleka proposal ikiitishwa ndo mr anafanya mambo ya invoice uongo??
haya turudi kwenye mada, siku hizi naona furniture centers nyingi zimemwagika na aina tofauti za sofa zinauzwa
kuna sofa za ngozi na hata zile za vitambaa lakin yenye material ya sofa nyengine zikiwa za rangi moja na nyengine zikiwa na maua ua au urembo tu wa aina tofauti
sasa pale mashost ukiwa nalo lile sio lazima upachike vitambaa vyako vya kufuma jamani au hata kama vitambaa redmade lakini usiweke kwenye hizi sofa
Ndo maana twaenda na wakati vitambaa vyako vile uvirembe kwenye yale makochi yetu ya mbao na mito ya sponch kwa wenye nayo.
Kwani haya ya sasa tayari yanaurembo wake ndo maana mwaona mchongo wake imerembwa, au aina ya kitambaa tayari imesharembwa ina maua au tangi zimepangiliwa kati ya mito ya kitambaa na sofa zenyewe....hapo kitambaa kina nafasi
badili ya kitambaa ukitaka kulihamasisha (kulipendezesha) basi tupia tumito twa umbo tofauti kopa, kisu na duara au vyovyote upendavyo...mwanamke ubunifu bibi ...kama si kwenda na wakati
Tipu:zile sofa za ngozi mwenzie AC....Pupwe...Kiyoyozi usije watoa watu vipele vya joto kwa kung\'ang\'aniza sofa za ngozi
 |

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala