PEDICURE!!
Saloon nyingi za kisasa hazijakamilika bila kuwa na kitu kinaitwa pedicure na manicure ila leo naomba niwadokeze kuhusu pedicure
Pedicure maana halisi ni uoshaji wa miguu kuanzia unyayo hadi kucha
Zipo mashine maalum kwa ajili ya pedicure japokuwa wengine hutumia beseni tu kwa ajili ya shughuli hiyo pevu
Kienyeji unaweza chukua beseni ukaweka maji na sababu ile ya maji pamoja na dettol kidoogo kisha unaloweka miguu kwa nusu saa.....au unaweka ndani ya hilo machine ambayo inakuwa kama inavibrate na kusaidia kumassage unyayo.
Baada ya miguu kulainika ngozi inakuwa imeshalainika na unaanza kusugua kutoa dead skin(Kitaalam) hivyo inaondoa ile ngozi iliyojichokea, kisha unasugua kucha pamoja na kutoa vinyama vya pembeni ya kucha.
Ukipenda unachukua scrub unasugua miguu na kisha unaifuta na kuipaka lotion na kupaka rangi ya kucha kama mpenzi wa rangi.
Hapo unakuwa nadhifu kuvaa sandoz
Vifaa hivyo vinavyotakiwa kwenye pedicure

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala