chumba cha mtoto!!
wow!! kama nawaona kina mama watarajiwa mnavyofurahia,
jamani chumba cha mtoto hakitakiwi kuwa butu kama lichumba la mama na baba kama si dada.
mandhali umeamua kumleta baby ulimwenguni huna budi kumkaribisha vizuri nae ajue anaingia ulimwenguni
haya kuna rangi kwa kila mtoto, kama mtoto wa kike basi vitu vya rangi ya pink ndo mwake kwake na kwa watoto wa kiume basi blue au njano au ikawa rangi zinasumbua atlist vitu vya rangi nyeupe plz
unaweza sema ni bei kubwa kupata vya read made lakini unaweza ona sample na ukampelea kwa fundi, picha za kubandika zauzwa rangi waweza paka hata mwenyewe. mradi chumba kibadilike
wapo wanafikiria labda nyumba ndogo basi hapo hapo kwenye chumba chako ila upande ule utakaoweka kitanda cha mtoto muwekee vipicha basi angalau
zaidi ya kuremba,mashuka yenye urembo za katuni, midoli na vitu vyake vya kuchezea kiasi kwamba hata akiamka anaweza akajisevia ye mwenyewe bila kukubugudhi.
Astaravistaa kwa leo!!

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala