Miss aliyechukuliwa ndivyo sivyo!!
Jina lake halisi ni Richa Adhia akiwa anahodhi miaka 19 Tangu alipozaliwa jijini Mwanza ambako aliishii mpaka mwaka wake wa 10 akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wanne
Akiizungumzia historia yake ya kielimu anasema amemaliza elimu yake ya sekondari katika shule ya Shaban Robert ya jijini na kimakazi anaishi Kariakoo na ni Katibu Muhtasi katika kampuni ya Berger Paints Ltd. (Robbialac).
Akielezea safari yake ya urembo anadai tangu akiwa mdogo aliipenda sanaa hii ila umri ndo ulikuwa kikwazo hadi mwaka jana alivyofanikiwa kufikisha miaka 18 ndipo alipojikita katika kuwania taji la BEAUTY QUEENS OF TANZANIA shindano linaloendeshwa na kampuni ya Compass Communication iliyo chini ya mkurugenzi wake Maria Sarungi
Niliposhiriki huko nilifanikiwa kushinda taji la Miss Earth ambapo nilienda nchini Philippines kuwakilisha nchi na alifanikiwa kuingia katika tano bora katika shindano la awali la Miss Bikini , ndipo kutokana na uzoefu nilioupata ndipo mwaka huu nikajaribu bahati yangu kuwania taji hili la Miss Tanzania
...nilianzia kitongoji cha Dar Indian Ocean ambapo nilishinda nafasi ya pili iliyoniwezesha niingine katika kinyang'anyiro cha kumsaka Miss Kinondoni niliposhinda kuwa Miss Kinondoni na kupata tiketi ya kuwania taji la Miss Tanzania....alisema Richa
Baada ya hapo nilishirki katika kinyang'anyiro cha MiSS Tanzania ambako nimefanikiwa kuvishwa taji na kutimiza ndoto yangU... Nilipotangazwa kuwa mshindi nilishikwa na butwaa na kwa sekunde chache niliona kama ni ndoto....
Akiongelea ushindi wake Richa anasema sio siri alishajipanga na kuamua na alikuwa na malengo hivyo alifanya jitihada zoote za kushinda kwa kuwa alishaamua kuingia kushiriki alikuwa anapigania kushinda
Kwa sasa Richa anajiandaa kuelekea nchini China mwezi ujao kwa ajili ya kushiriki kinyang'anyiro cha kumsaka Mrembo wadunia 2007 katika shindano litakalofanyika Sanya nchini China
Kwa mujibu wa Lundenga alisema kuwa Richa anavipaji lukuki ikiwemo kucheza soka, basket ball na pia ni muogeleaji mzuri na tayari ameanza kujifua vilivyo ili aenda kushiriki shindano la vipaji pamoja na lile la Beuty with purpose ambapo mshiriki huangalia ameifanyia nini Jamii
Mbali na Hayo Richa amejikoki vilivyo katika kuitangaza Tanzania ambapo ana mambo haya matano aliyojiandaa nayo iwapo ataulizwa kuna nini Tanzania bila kufikiria atawajibu hivi
(1)Amani na Upendo: Nchi yetu ina makabila mengi na kila kabila lina utamaduni wake. Lakini tunaishi pamoja kwa amani na upendo pia tuna uhuru wa kuabudu.
(2)Tanzanite: Ni nchi pekee duniani yenye madini ya Tanzanite.
(3)Ngorongoro crater: Hii ni maajabu ya nane ya dunia na ipo Tanzania.
(4)Mlima Kilimanjaro: Ni mlima mrefu kuliko yote Afrika. Ni kivutio kikubwa kwa watalii.
(5)Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika: Ziwa Victoria ni ziwa kubwa kuliko yote Afrika, na Ziwa Tanganyika ni ziwa lenye kina kirefu kuliko yote Afrika.
Nilitaka kujua Richa alipokeaje ushindi wake na kupingwa kwake na baadhi ya wadau wa urembo wakiwepo warembo waliwahi kuhodhi taji hilo
......Nashukuru sana, mimi ni Mtanzania mwenye asili ya kiasia, lakini nimezaliwa Tanzania na wazazi wangu wamezaliwa Tanzania, mama yangu anatoka Pemba na baba yangu anatoka Morogoro. Nimekulia katika utamaduni wa kitanzania, ni utamaduni pekee ninao ufahamu, ninaouthamini, na ninao upenda kwa dhati.
Nawaomba watu wa kundi hilo wanaonipinga, waungane na mimi wanipe sapoti kwa sababu ninawakilisha Watanzania wenzangu wote......Ni hayo tu ambayo Richa aliweza kusema.
Wapo wengi walihoji Vije Richa ambaye anadai mama yake mpemba na babayake ni mtu wa Morogoro lakini alisalimia kisukuma siku ileee ya mashindano...anadai ye aliishi Mwanza hivyo akawa ameinyaka hiyo lugha.
Mbali na huu Umiss pia Richa anafanyaga modelling uanamitindo (Modelling) ambapo anadai ye alianza kufanya hiyo tangu mwaka 2004 ambapo mbunifu Mustafa Hassanali ndie aliyemuibua na ndio anayefanyaga nae kazi hiyo...na hadi leo anasema ndie mbunifu anayemvisha na anaamini test yake
Nilitaka jua kama Familia yake inampa support gani kwenye hii fani
Alisema Familia inampafull support akiwepo mama yake ambaye anampa shavu la kutosha, bila kumsaha dada na kaka na Nana 'bila shaka anamaanisha bibi yake'
Akielezea hobby zake anasema anapendelea saana kusoma, kucheza, kupika kusafiri pamoja na kupumzika pembezoni mwa bahari
Anamuelezea baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama mtu anayemuadmire na kwa kuwa mstari wambele kudai uhuru wa Tanzania na kutetea ubaguziwa rangi
Anamuelezea Mama yake kama mtu anayenihamasisha kwa kila kitu ikiwemo ushauri moyo ni zaidi ya mama kwani ni kama rafiki yangu mpenz
Richa alikuwa na ujumbe kwa wasichana wenzie ambapo aliwaambia kuwa wao ndio watakayoyaunda maisha yao na wo ndio watakayoyanyoosha au kuyapindisha hvyo hawana budi kuwa makini na kutomruhusu mtu yeyote kuyaingia maisha yao...wote tushikamane na tujifunze kutokuwa tegemezi
Darhotwire inamtakia kila la kheri Richa aweze ipeperusha bendera ya Tanzania vizuri

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala