Tafuta DHWTangazaTuandikie
Kiburu

MAHITAJI

a/ Ndizi mshare
b/ Maharage
c/ Magadi
d/ Kitunguu

NAMNA YA KUTAYARISHA PAMOJA NA UPIKAJI WAKE

a/ Kwanza kabisa loweka magadi kama vijiko 2 vya chai kwenye kikombe,
b/ chemsha Maharage yako kiasi kinachotegemea na ndizi zako ni kiasi gani
ila hakikisha hayo Maharage yasiive sana.
c/ Wakati maharage yako jikoni endelea kumenya ndizi zako za Mshare na kisha uzikatekate ndogondogo pembe nne(squre).

d/ Baada ya kuandaa vyote hivyo, chukua sufuria yako ukipenda kuanza na maharage au ndizi yote ni sawa.
e/ Weka maharage ndani ya chombo chako cha kupikia, katia kitunguu 1, ndizi ulizoziandaa.
f/ Usisahau kuweka mafuta na chumvi kiasi kwani bila hivyo chakula hakita faa kuitwa chakula.
g/ Ukimalizia kuweka vyote hivyo, mwisho malizia kwa kuweka magadi uliyoyaandaa pamoja na kiasi cha maji.
f/ Mwisho chukua sufuria yako yenye michanganyiko ya hicho chakula na kisha ubandike jikono.

Haya wenzangu kama mnavyoona baada ya muda chakula chetu kitakuwa teyari, na ukishakiepua kutoka jikoni bandika maji yako ya moto kiasi.
Huku maji yakiwa jikoni endelea kukiponda chakula chako kwa kutumia mwiko na baada ya hapo endelea kuweka maji kidogo kidogo kwenye chakula hicho mpaka pale kitakapo kuwa kizito kiasi na baada ya hapo ndipo hufaa kuliwa.



Imeandalia na Jacque


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.