Tafuta DHWTangazaTuandikie
Meza gani hufaa kwa Chakula?

Kila mmoja wetu hupenda kuwa na kitu kizuri na kinachoifanya nyumba yake iweze pendeze na iweze kuvutia kwa zaidi, pia kwa upande mwingine unaweza ukawa na vitu vizuri na vya thamani lakini baada ya kuipendezesha nyumba yako unaifanya kuchukiza a kukosa mvuto kabisa.

Meza ya chakula ni kati ya vitu muhimu kwenye nyumba yoyote ile, kwani wakati wa familia ni wakati wa kukusanyika pamoja.

Ni familia chache sana huwa wanapenda kukaa pamoja mezani kwa kula chakula pamoja nafamilia zao, lakini wengi wao ifikapo muda wa chakula huwa kila mmoja hujipakulia chakulachake na kujimuvuzisha kivyake.

Leo katika safu hii ya nyumba tunazungumzia nini unatakiwa kufanya ili kuweza kutambua meza ipi ya chakula inayoweza kupendezesha nyumba pamoja na chumba chako cah kulala (Dining Room).

Kwanza tambua kabisa chumba chako ni cha ukubwa wa aina gani kwani kunaumuhimu mkubwa sana wa kutambua hili, kwani unaweza kununua meza ndogo wakati chumba chako ni kikubwa hivyo hupelekea chumba kupwaya zaidi.

Pia unaweza kununua meza kubwa wakati chumba chako ni kidogo, hivyo kukosa hata sehemu ya kupita kutokana na nafasi ya chumba kuwa ndogo kwa sababu ya ukubwa wa meza yako uliyoinunua.

Ni vizuri wakati wa kununua meza ukatambua kuwa familia yako inaidadi ya watu wangapi, kwani unaweza kununua meza ndogo na huku familia yako inaidadi ya watu sita kwani inakuwa haipendezi wengine kukaa mezani na wengine kukaa jikoni kwani kama watu ni wengi katika familia yako usinunue meza ndogo kwani haitoshelezi.

Ni lazima lazima ufikirie umuhimu wa kuwa na meza kubwa ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza iwapo haitatoshelez familia yako, na pia ni vizuri ukawa na meza ambayo ina viti viwili vya ziada kwa ajili ya wageni.

Baada ya kutambua hayo sasa unaweza kwenda dukani na kununua meza yako ya chakula.



Mwana mke pambo bwana katika nyumba!!nadhani umenipata ipasavyo, kazi kawo..bye


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.