Tafuta DHWTangazaTuandikie
Mboga ya karanga

MAHITAJI

a/ Sufuria Mwiko mdogo
b/ Maji kiasi ambayo yanahitaji wingi wa mboga yako
c/ Chumvi
d/ Brenda/Kitwangio
e/ Nyanya chungu, Mafuta ya kupikia, Kitunguu kikubwa 1 na kisu.

NAMNA YA KUTENGENEZA

a/ Saga karanga katika brenda yako au twanga katika kitwangio na mapaka zilainike vizuri,
b/ menya nyanya chungu na uzikate kate katikakati na kisha menya kitunguu na ukikatekate.
c/ Chemsha maji kisha yaweke katika chombo kisafi kisha weka mafuta katika sufuria yako na kuyainjika jikoni, yaache yachemke kiasi kisha weka kitunguu hakikisha kinaiva vizuri hadi kiwe na rangi ya kahawia.
d/ weka karanga na nyanya chungu uzikaange mpaka ziive vizuri.

Chukua yale maji uliyoyachemsha ambayo bado ni ya moto, uyaweke kwenye mchanganyiko wa karanga na nyanya chungu, weka chumvi kisha endelea kukoroga kwa kutumia mwiko bila kuacha mpaka mchanganyiko huo uive vizuri.

Unatakiwa kukoroga muda wote mboga inapokuwa ikichemka ili isiungue, pia unashauriwa kutumia maji moto ili mboga yako isiwe na harufu ya karanga mbichi na baada ya muda itakuwa teyari kwa kuliwa haswa na ndizi pia huweza kutumika kulia ugali au wali.




Imeandaliwa na Jacqueline


 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved.Design by Infocomtechnologies Limited.