KEKI YA NYAMA (MEAT CAKE)
MAHITAJI
a/ Nyama kilo 1 1/2 (ya kusaga)
b/ Siagi 1/4kg
c/ Unga1/4kg
d/ Carrot 1/4kg
e/ Pilipili mbuzi 1/4kg
f/ Mayai 18
g/ Mdalasini
h/Pili pili manga
i/ B.powder 2tsp
j/ Ndimu 1
NAMNA YA KUPIKA
Changanya nyama, ndimu, pilipili manga, mdalasini na upike
pamoja viive, saga siagi na mayai 6 hadi iwe cream na nyepesi kama
unavyofanya kwa keki ya sukari.
Changanya pamoja kwa unga na B.powder changanya kwa mkono mpaka uchanganyike koroga mayai mengine 6 na uchanganye na ile nyama kwa kijiko mpaka ichanganyike vizuri.
Kwangua carrot zako kwa kutumia kile kibati cha kuparia chips nazo ziwe kama chips
tena zichemshe kidogo ziive, kata pilipili ziwe slices za duara nyembamba.
Mwisho paka trey yako siagi itandaze ienee yote na mimina ule
mchanganyiko wa cake juu yake halafu tandaza juu yake ule mchanganyiko
wa nyama na mayai.
Tena vunja mayai 6 yalibakia uyapige vizuri, tandaza carrots zako juu yake na zile slices za pili pili boga kisha malizia kwa kunyunyiza yale mayai uliyoyapiga weka katika oven pre-heated temp. 180C mpaka ikauke na iive na ikipoa kata square na uwandae.
Imeandaliwa na Jacqueline

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala